NAJMA SEHEMU YA TISINI NA NNE(94)
Story..........NAJMA(94)
Mtunz.......KING SOKA
Phone. .....0717758864/0786604915
Page..........Hadithi kali za kingsoka
Albam...... BORA NIENDE
************UJUMBE TU
ukiishi sehemu za watu usiishi jinsi utakavyo mpaka ukawa
chukizo kwa wale wakuzungukao.
Ishi kwa kujitahidi kumfurahisha kila mtu, japo uwezi
lakini jitahidi.
Hata mimi natambua wapo wanaopenda , na wasiopenda lakini
najitahidi wapende.
Dharau na kejeli ni adui katika jamii inayo kuzunguka,
usimzarau fukara kisa unamzidi kipato.
SONGA NAYO....
"hapanaaaaa! Usifanye hivyooo....."
Sauti ilisikika ikitoka katika moja ya gari iliokuwa
ikikatiza maeneo yale, ndani yake pakiwa na watu wawili .
Alikua ni Deo ndani yake akiwa na Candy msichana aliekuwa
ni mpenzi wa Rashidy lakini aliondoka baada ya Deo kusema ukweli mbele yake.
"Deo unakumbuka alivyo kufanyia pake ndani kwake,
achana naye Dunia imfunze maana ndiyo mshahara wa dhambi"
"Hapana Candy, usilipize baya kwa baya hata vitabu
vya dini vinahusia sana swala hilo, ni vyema tumsaidie, anaweza akafa hivi hivi
wewe siunaona lile jiwe lilivyoshikwa na yule jamaa, tena anaonyesha hana hata
chembe ya utani, mbaya zaidi hakuna anaemsaidia"
Deo aliongea kwa sauti ya upole sana, akionyesha roho ya
kumsaidia rafiki yake, japo muda mfupi walitoka kukwaruzana na kufikia
kutukanana.
"Mmmmh! wale vijana hawampendi kuliko mtu yeyote.
Siku moja aliwamwagia maji katika lile dimbwi pale, alafu
akawatukana pia, ndiyo maana hata Mungu anamuhadhibu eneo hili pia vijana wale
wakishuhudia. "
Candy aliongea lakini muda huo Deo alikua ameshashuka
ndani ya gari, akipiga hatua chache kuekekea alipo Rashidy na mtu aliyekuwa
aneshikilia tofali kwa juu akitaka kumpiga Rashidy kichwani.
"We kunguru unatokea wapi? Unajua chanzo cha uo
ungomvi au shobo zako tu ili uonekane umefanya msaada.
Acha uduanzi wewe boy* tutakuamkia na wewe sasa hivi,
unajua ni kiasi gani mwana huyo alivyo umia au?"
Vijana wale kwa jaziba waliamka huku maneno makali pamoja
na matusi yakiwatoka.
"Hapana Kaka zangu, msifanye hivyo.
Mimi nawafahamu, na natambua ni kwa nini mnamchukia
kijana yule, lakini msameheni ajui hatendalo.
Pale alipo ahata yule anaeenda kumsaidia tayari amesha
tibuana naye, hata mkimtizama usoni anamakovu ya ngumi alizopigwa na kijana
yule.
Nakumbuka aliwamwangia maji machafu huku akiwatusi siku
moja, naomba mumsamehe pale alipo anatafuta pakufia."
Candy alikua ajiongea na vijana wale waliokuwa na kila
dalili za kwenda kumzuru Deo kwa kutaka kutoa msaada kwa Rashidy.
"Kumbe siku ile na wewe ulikua, ndiyo ulikuwa ukimpa
kiburi.
Sasa na wewe kwanza utakuwa halali yetu ndipo yule
tumsamehe, chagua moja sasa.
Maana nyie mademu(wasichana) mkiwa na mabwana wenu katika
gari mnakuaga na nyodo sana, sasa leo utajua kama maharage ni mboga ya Taifa.
Mlitutukana sana ile siku"
Mmoja wa vijana wale aliongea uku akiwa anawatizama
wenzake, kwa kuonyesha wapo pamoja.
"Sawa nyie fanyeni mnachotaka, kwani sindiyo mlivyo
amua.
Lakini yule mimi siyo mpenzi wangu japo alikua hivyo lakini kwa sasa siyo.
Ni kijana asiyekuwa na malengo yupo kama taira aliepoteza
dira, ndiyo maana mnamuana vile pale
hata mkimpiga mtakuwa mmempunguzia hadhabu"
Vijana wale walicheja sana, uku wakimshika Candy kichwani
kumtoa wasiwasi.
Wakimwambia awe na amani.
"Kuwa na amani sister(Dada) sisi siyo vijana wahuni
kiasi hicho, ika bwana ako ndiyo
alitufanyia uhuni"
Baada ya Deo kufika pale, wakati huo Rashidy akiwa
amepiga magoti akiomba msamaha usiosiklizwa, alipo muona Deo alihisi kama
amemuona Mungu wake.
"Hafadhali kaka umekuja kuniokoa nakufa mwenzako
nakufa, nisaidie nitoke hapa mengine tutaongwa nyumbani"
Rashidy aliongea huku akitaka kunyanyuka baada ya kumuona
Deo.
"Mimi siyo kaka yako, hata undugu na wewe sina leo
hii nakuaje Kaka yako?
Umesahau muda mfupi umenipiga na ngumi za kutosha mpaka
imenibidi nipitie hosptali kwanza, wewe endelea na mambo yenu ila mimi hapa
nimekuja kuomba akufanye chochote ila gari asiiguse maana siyo mali yako"
Deo akiongea huku mikono ikiwa mfukoni, akiashiria hajaja
kuomba msamaha kwa ajili ya Rashidy bali kwa ajili ya gari.
"Hapana kaka huyu mtu ataniua mimi, siyo mtu mzuri
hata kidogo amini nakuambia Deo.
Upo tayari mimi nife kwli, umesahau mangapi mimi
tumefanya na wewe mpaka leo unaniacha katika hali kama hii.
Usifanye hivyo, mimi ni mkosaji lakini usinihukumu kiasi
hiki mimi nisamehe Deo, sidudii tena ndugu yangu nakufa najiona, au nitakuwa
kilema mwenzako"
Rashw aliongea mpaka analia lakini Deo akuonyesha hata
dalili ya kumjali.
Zaidi ndiyo kwanza alitoa simu yake akiwa anampiga picha
jinsi alivyokuwa chini akiomba msamaha.
Na kumrecod video jinsi anavyolia.
"Nilikuambia wewe, utaishi kama mbwa koko ona sasa,
hata siku haijaisha umesha changanyikiwa kiasi hiki.
Kufa huto kufa lakini chamoto utakiona amini nakuambia
yani ni lazima utatafuta mlango wa kutokea lakini itakiwa imefungwa.
Pole sana Rashidy rafiki yangu wa zamani, nilikuoenda
sana lakini sasa kila moja afe kivyake.
Candy mamy tuondoke zetu acha afe, atufai huyu mimi
siwezi kumsaidia ile hali mwenyewe nina matatizo yangu"
Deo aliongea huku akiwa anageuka kuondoa zake katika gari
yake
ITAENDELEA.............
Jifunze kupitia
mimi.
Maisha ni safari ndefu yenye kila kitu kona nyingi.
Ukinyooka usisahau kama mbele kuna kona yasikukute ya Rashidy.
UJUMBE TU
SOMA KWANZIA 95 MPAKA MWISHO KWA TSH2000
WHATSSAPP
LIPA KWA NAMBA HII 0717758864
TEXT WHATSAPP 0717758864