BORA NIENDE SEHEMU YA SITA
BORA NIENDE(6)
KING SOKA
PHONE:+255717758864
DAR ES SALAAM_TZ
PAGE
#STORY_ZA_KING_SOKA
Email address
jacksonsoka@gmail.com
Nilimpita na kuelekea
chooni na kwenda kumaliza matatizo yangu huko kisha kuingia jikoni uku nikiwa
na njaa kweli nilijipikia chai ili nipate nguvu ya kutoa hukumu.
Sikitaka kutua vitu
alivyokuwa kaviandaa mkewangu kwa hofu ya kuweza kuniwekea sumu au hata kitu
chochote cha kunizuru.
"Mume wangu
wangu chai nimesha weka mezani mbona unaingia jikoni peke yako.
Siwezi kukuwekea sumu
mume wangu wangu maana huna kosa lolote ulilo nitendea ninaestahili azabu ni
mimi hivyo ondoa shaka nenda kanywe chai ipo mezani nimesha kuandalia"
Aliongea mke wangu
huku akiwa amepiga magoti.
Sikumjibu kitu
chochote zaidi ya kimtazama usoni tu jinsi alivyokuwa akitia huruma.
Maana kila nilipo
muangalia usoni nilibaki kulia mimi kwa uchungu uliyo changanyika na asira
ndani yake.
"Mke wangu nini
hasa nilicho kukosea mpaka ukaamua kunitenda kihasi hiki, cha kunifanyia
nijutie maisha yangu, ni kwa nini nilikubali kukuowa na kuishi na wewe.
Unajua fika kila
nilichokifanya ni kwaajili yako hata maisha yangu nilikua tayari kuyatia hatarini
ili mradi wewe ufurahi na ujue unaye mwanaume anaekujali nakukusamini iweje leo
unifnyie hivi.
Hivyo naomba niache
kwanza nifanye mambo yangu pia nijiandalie chai na maji kisha nioge.
Nikisha maliza kuoga
ndipo tutaongea vizuri.
Umenifanya niwe mtu wa
kulia kila kuitwapo leo unazani ni kwa nini mimi nimekuwa ni mtu wa kujutia
sasa maisha yangu.
Unajua nimesha teseka
sana juu ya maisha yako nazani unalitambua hilo.
Ulipatwa na ajali na
huo ndiyo ulikua mwanzo wa mimi na wewe kukutana.
Pia ajali uliyoipata
ulikua ni mtu wa kufa maana hata msaada ulikua hauna zaidi yakugaragara chini
huku ukiwa unatokwa na machozi huku mwili mzima ukiwa umelowa damu.
Na pahali ulipokuwa
ilikuwa ni vigumu sana wewe ukuonekana nai mtu wa aina yeyote hata mimi ni
bahati tu kukuona maana hata njia hile nilikuwa siipitagi ninapotoka
kibaruani kwangu.
Usione mimi
nimeshindwa kufanya lolote ukazani labda nimeogopa hapana.
Unakumbuka ulivyopata
ajali ni nani alikusaidi ujui unakumbuka ni maeneo gani?
Naomba niache"
Niliongea kwa uchungu
sana huku nikishindwa hata kumtazama mke wangu usoni maana nilitamani hata
kummeza kila nilipo muangalia usoni na jinsi alivyokuwa anatia huruma.
"Vipi dada
umepatwa na nini na mbona mwili mzima umetapakaa damu, inanekana umepata ajali
na umekuja kuterakezwa hapa maana hii njia hata pikipiki huwa hazifikagi.
Wewe umefikaje jamani
hapa maana sijui hata nifanye nini kukusaidia na mimi nipo na baiskeli yangu
nitakubeba vipi kukupeleka hosptali maana hapa ni ngumu kupata msaada"
Niliongea mimi siku
ambayo nilikua nikitoka kibaruani kwangu siku hiyo nilikua na shift ya kuingia
saa tisa mchana na kutoka saa tano usiku.
Katika kiwanda cha
maji na mikate alimaarufu kama Azam.
Nilistuka kukutana na
mwanamke akiwa amelowa damu mwili mzima na hata sauti ikiwa aimtoki.
Kila nilichojaribu
kumuuliza bado alishindwa hata kunijibu zaidi ya kugaragara chini.
Nilimuonea huruma na
kuamua kumchukua na kumbeba mgongoni huku nikimkimbiza kuwahi hospital ya
temeke.
Yalikua ni maeneo ya
tazara eneo liitwalo Mchicha ndipo nilipo mkuta msichana huyo aliyeonekana kuwa
amepata ajali na kuja kuterekezwa huku makorongoni huko akiwa hana hata msaada
wa aina yeyote ile.
Baada ya kutembea kwa
umbali mrefu kidogo ilitokea bajaji iliyokuwa ndiyo msaada wangu na kunisaidi
kumbeba msichana yule huku mimi nikiwa ndani yake .
Baati nzuri tulifika
hosptali ya temeke mwanamke yule akiwa bado anapumua tulipokelewa vizuri na
manesi waliokuwa zamu huku Doctor nae akiwa karibu haikuchukua mda tayari
alisha kimbizwa chumba cha wagonjwa mahutihuti na huduma ya kwanza na kazalika
zikaendelea.
Huku mimi nikiwa
nimebaki nimekaa katika bench la hosptalini hapo nikisubiri najibu ya Doctor
nijue cha kufanya kama niondoke na kurudi asubuhi au nilale hosptali hapo.
"Habari yako
kaka wewe ndiye mliyekuwa na dada aliyepata ajali"
Aliniuliza nessy wa
hosptal ya temeke.
"Ndiyo ndiyo
mimi niliye mleta, kifupi ni magonjwa wangu.
Nolimjibu nessy
"Nasikitika kukuambia
mgonjwa wako ana hali mbaya sana, hivyo inabidi aongezewe damu kwanza kabla ya
yote, maana ametokwa na damu nyingi sana na pia nikupongeze kwa kumuwahisha
hospitalini hapa, maana ungechelewa kidogo usingekuwepo naye tena duniani kwa
jinsi alivyo tokwa na damu nyingi"
Aliongea nessy yule
na kunifanya nijikute nikitetemeka mwili mzima kwa kuwaza ni vipi nitapata damu
ya kumuongezea mgonjwa huyo ikiwa ni tayari mgonjwa wangu na ndiyo niliempelea
hosptal nikiwa simfahamu wala hata ndugu zake siwafahamu.
"Niache mbona
unanizuia nini nisiongee we niache nikukumbushe maana najua hujui mke wangu
nilipo kutoa au ni wapi ulipotokea ungelikua unajua using fanya haya hivyo
niache niongee.
Usitake kunikorofisha
sawa"
Niliongea huku nikiwa
na hasira sana kiasi nilikua nikitetemeka wakati namkumbusha mke wangu jinsi
ilivyokuwa.
ITAENDELE→→→→→→