BORA NIENDE SEHEMU YA KWANZA
BORA NIENDE(1)
KING SOKA
+255717758864
“Oooooh ashhhhhh.
Yeeh oooooh
Uuuuuuuw
Inatosha tamu,
ulikuwa wapi ! siku zote hizi atukufahamiana.
Jamani uwii
unanafikisha penyewe, wewe ni mwanaume wa ajabu sana.
Ni moja ya sauti
niliyoisikia ikitoka ndani ya nyumba yangu, na baada ya kuisikiliza kwa makini
niligundua ni mke wangu ameamua kuingiza mwanaume ndani kwangu.
Nilibaki nikisikiliza
na kushindwa hata kupata maamuzi ya nini nifanye “.
Nilijikuta nikiihiwa
nguvu mpaka kujikuta natereza na ukuta mpaka chini.
Kwakuwa ilikua ni
usiku na nilikua nimetoka safari nimechoka nilijikuta nikilala njee bila hata
kuingia ndani kwa jinsi nilivyojisikia uzuni na kuchoka kwa kusikia mke wangu
akiugumia mapenzi na mwanaume mwingne tena ndani kwangu ilinifanya nijione kama
mjinga niliedhindwa kuilinda familia yangu na kuona ni moja ya zarau kubwa sana
maishani mwangu.
Nilivumilia mpaka
asubuhi nilishuudia kwa macho yangu, mpenzi wangu akimtoa mwanaume yule mpaka
njee ya geti.
Niliinuka taratibu
kutoka nilipokuwa nimejifika na kuingia ndani kimya kimya.
Kutokana na mlango
kuuwacha wazi wakati wakitoka njee na mwanaume aliona ndiye anaemfikisha alipo
pataka na kuniona mimi mi kama mjinga mpaka kuniletea mrisi ndani ya nyumba
yangu.
"Mwanamke wangu
huyu au naota kweli anafikia atua ya kuniletea mwanaume ndani ya nyumba yangu
kisa kujua nimesafiri, takribani mwezi sipo atakuwa kalala na wanaume wangapi
katika kitanda changu mimi.
Hanifai mwanamke huyu
bora ya lawama kuliko fezea.
Siwezi fanyiwa hivi
na mimi nikakubali.
Nimetoka safari kwa
furaha lakini now nakuja kukutana na haya ni bora angefanyia huko njee na
nyumba ninayo lipa kodi mimi.
Haiwezekani mimi kuwa
mjinga kiasi hiki bora niondoke na kwenda kuitafuta amani mbele kwa mbele"
Niliwaza sana baada
ya kuingia ndani nikiwa nimeketi sebuleni.
Niliamua nitoke njee
na kujificha nilipolala usiku kucha.
Nilimshuudia mke
wangu akirudi ndani uku akiwa na vazi moja tu yani kanga pekeyake.
Nilimtazama sana mke
wangu kwa jinsi
nilivyokuwa
nikimgaramia alafu kumbe kuna mjinga anatembea nae iliniuma sana.
Nilimua kuchukua vitu
vyangu nilivyotoka navyo safari na kutoka taratibu nikafungua geti na kuondoka
uku moyoni nikiuzunika sana.
Sikuwahi kutegemea
kama mke wangu anaweza nifanyia hivyo kwa jinsi alivyokuwa mtu wa dini, na
masaa yote alipokuwa na mda uwezi mkuta akiwa amekaa bila kuwa na vitabu vya
dini, au akiimba nyimbo za dini.
Kila nilipokuwa
nikiambiwa na marafiki zangu nilikia nikibisha kumbe nilikua najichimbia kaburi
pekeyangu.
Hata kisa cha
kugombana na jirani tangu Mr Joseph ni kutokana na kuniambia habari za mke
wangu ajatulia, na kila mara huwa anamkura na watu tofauti tofauti katika bar
hata barabarani.
Pia aliendelea
kuongea akisema madereva pikipiki nao walikuwa wakimchukua mke wangu bado
akusita kuendelea kuongea pia bosi wa mke wangu anatoka na mke wangu,
Nilikasirisha na
kauli za Mr Joseph na ndipo uzalendo ulinihinda na kujikuta nampiga jirani
yangu na kumzalilisha sana tena mbele ya mke wangu na mke wake na majirani
wengi waliokuwa wamejazana kushuudia ugomvi uwo.
Kumbe nilikuwa
nikikosea sana na mbele ya mke wangu naye alinisaidia kumpiga jirani yangu Mr
Joseph.
Kumbe alikua akificha
makucha yake yasijulikane na watu.
Nakumbuka mr Joseph
aliniambia maneno machache tu ambayo ndiyo haya ninayo yashuudia leo.
"Jack!
Umenizalilisha vya kutosha, ila ipo siku utakuja kunikumbuka na kutaka kuniomba
samahani lakini utakuwa umesha chelewa? na utajuta nakuambia amini maneno yangu
na yatakufanya ulie na kusaga meno.
Narudia tena
kukuambia huyo siyo mwanamke wakuishi naye"
Aliongea Mr Joseph
huku akitokwa na machozi mbele ya umati wa watu wasiyo pungua mia(100+) na
zaidi, sikuwa na hata chembe ya uruma kumsamee mwanaume mwenzangu.
Nilifurahi kumuona
mwanaume mwenzangu akizalilika mbele ya umati wa watu wakiwemo wengi wao ni
wanawake tena wauswahilini.
Baada ya kutoka
getini niliamua kuondoka mpa kinondoni ambapo niliamini huko ndipo nitaweza
kupata nyumba au hata chumba ambacho niliona naweza kuishi na kuanza maisha
mapya na badae kwenda kumchukua mwanangu.
Maisha mapya nilianza
kinondoni nikiwa mimi kama mimi na kunifanya mtaani kuonakana ni kijana mkubwa
nisiye kuwa na familia ikipelekea baazi ya vijana kupendelea kuja kwangu kupiga
story za msisha nk.
Maisha yalizidi
kusonga mbele huku nikiwa bado namtumia mke wangu
pesa za matumizi
kwaajili ya mwanangu na yeye pia.
Kwa kipindi chote
tayari ilishapita miezi miwili nikiwa bado hata sijamwambia mke wangu kama nipo
Dar es salaam.
Ilibaki kuwa siri
yangu kujua nilipo na sikutaka kumwambia kwani nilishazamiria kuachana naye
kabisa na sikutaka hata mawasilino naye hata kidogo kwa ukatili alo nifanyia
ulikuwa ukinitesa sana moyoni kila nikikumbuka ilifikia mpaka kipindi
nilitamani kunywa sumu bila hata kujali kutonana na jinsi nilivyo mpenda mke
wangu.
Kilichoutesa moyo
wangu ni pale nilipo kumbuka maneno ya mr Joseph.
Yalikua yakiitesa
sana akili yangu.
Siku moja nikiwa
nimekaa, nyuma ya nyumba niliyokuwa nimepanga, nilisikia simu yangu ndani
ikiita, niliinuka haraka kuifuata lakini baada ya kuipokea simu nilijikuta
nikishindwa kuvumilia na kuamua kuondoka haraka.
ITAENDELEA. .....