Michezo Tarajia kumuona Fosu-Mensah Old Trafford hadi 2020
Man United katika harakati za kuendelea kuboresha timu yao katika mashindano tofauti, October 19 2016 Man United imetangaza kumpa mkataba mpya beki wa kimataifa wa Uholanzi aliyejiunga na Academy yao 2014 Timothy Fosu Mensah.
Fosu-Mensah mwenye asili ya Ghana amepewa mkataba mpya na Man United utakaomuzesha kusalia Old Trafford hadi 2020, Fosu-Mensah ambaye ana uwezo wa kucheza nafasi ya beki na kiungo mkabaji alijiunga katika academy ya Man United akiwa na umri wa miaka 14.
Nyota huyo kwa mara ya kwanza kuichezea Man United katika mechi ya Ligi Kuu England ilikuwa ni msimu uliopita dhidi ya Arsenal, hiyo ilikuwa ni baada ya kucheza katika kikosi wachezaji wenye umri chini ya miaka 21, Fosu Mensah ameichezea Man United michezo 12.