BORA NIENDE SEHEMU YA PILI
BORA NIENDE(2)
KING SOKA
PHONE
+255717758864
Siku moja nikiwa
nimekaa, nyuma ya nyumba niliyokuwa nimepanga, nilisikia simu yangu ndani
ikiita, niliinuka haraka kuifuata lakini baada ya kuipokea simu nilijikuta
nikishindwa kuvumilia na kuamua kuondoka haraka.
ENELEA. .........
Niliamua kuondoka
haraka kufuata taarifa niliyoipokea kupitia simu niliyo ipokea kutoka kwa mtu
ambaye bado nilikua sijamfahamu hata kwa sauti ilikua ni ngeni masikioni
mwangu.
"Hallo vipi
bwana mkubwa! Samahani wewe ndiye jackson?"
Aliongea mtu
aliyenipigia simu
"Ndiyo
mimi"
Nilimjibu
"Samahani kwa
raarifa hii ninayokupa, wewe ndiye unayeishi namba kp134 na ndiye unafamilia
hapa lakini nimesikitika sana kwa tabia za mke wako za kila siku kuingiza
wanaume ndani yani nyumba imekuwa kama gest.
Na mbaya zaidi yupo
na mtoto mdogo wa kike naimani ni mtoto wako.
Hivyo mimi kama Baba
mwenye nyumba nataka mara moja muhame katika nyumba yangu mnaitia aibu nyumba
yangu kwani guest azipo au kisa mnaona nyumba nzuri ndiyo mnatumia mtakavyo
kama unataka kuamini njoo sasa udhuudie mwanaume mwingine yupo ndani
kwako"
Aliongea mtu yule
aliliye jitambulisha kuwa ni baba mwenye nyumba yangu, lakini hakuwa yeye hata
sauti wala namba haikuwa yake.
Mda mfupi baada ya
kupokea simu nilishawasilisi sted ya daladala maarufu kama Mananya na kwa baati
nzuri sikukaa muda mrefu nilipata gari ya kuelekea gongo la mboto.
Nilikaa katika siti
huku nikiwa na mawazo sana, nitaweza kuvumilia kweli fumanizi nitakalo likuta
mbele ya macho yangu tena kutoka kwa mwanamke niliyempenda na kumfungulia mradi
SALOON kubwa ya kisasa duka la nguo huku bado nikizidi kumjali kwa vitu
vingine.
Nilikaza moyo na
kujisemea moyoni liwalo na liwe kisha nikachukua simu yangu na kuplay mziki na
kuanza kusikiliza taratibu, niliukumbuka mwimbo wa Rich mavoko_roho yangu.
Huku machozi yakinitoka.
"Kweli kuchapiwa
ni siri ya ndani lakini kwangu hii ni zaidi ya fedhea.
Nyumbani kwangu,
shuka langu, taulo langu mpaka kitanda changu yani mtu anavitumia mimi siwezi
BORA NIENDE kuishi mbali naye nimuachie nafasi ya kujiachia na hao alio waona
ni waumuhimu sana kuliko mimi, uwenda wanamfikisha zaidi yangu siwezi jua mimi
ni mwanadamu sijakamilika"
Nilijikuta nawaza
mpaka machozi yakinitoka na kujitahidi kuyafuta ili kupoteza ushaidi nk.
"Kaka vipi mbona
unalia peke yako una matatizo gani?"
Aliniuliza abiria wa
pembeni yangu niliekuwa nae siti moja.
"Hapana nipo
sawa, ni matatizo madogo tu si unajua tena binadamu sisi misukosuko ya hapa na
pale kawaida hivyo ondoa shaka dada angu"
Nilimjibu huku mimi
nikijiandaa kushuka standi ya daladala njia panda air port.
Nilichukua usafiri wa
haraka bodaboda na kuomba anipeleke karakata ilipoku nikiishi na familia yangu(
mke wangu na mtoto wangu.
Baada ya kufika
nyumbani kwangu na familia yangu niliamua kutumia akili ya kuzaliwa.
Kwakuwa nyumba hile
ilikua na geti hivyo nilamua kuzunguka nyuma ya nyumba na kuruka ukuta na
hatimaye nilidondokea ndani ya fensi.
Haikuwa kazi kubwa
sana kuingia ndani, kwani hata mimi nilikua na ufunguo wangu, niliokuwa
nikiutumia kama funguo ya zarura bila hata mke wangu kafahamu hilo, nilifungua
mlango taratibu na kuingia mpaka ndani sebleni, na kuamua kukaa kwanza huku
nikijipanga jinsi ya kuingia chumbani kwangu na kuweza kupambana kwa hali
yoyote ilakayo tokea, huku nikiwa na begi dogo mkononi ili nionekanane kweli
nimetokea safari tena nikiwa najifanya kama sijui kilichokuwa kinaendelea, huku
nikiwa na zawadi kidogo nilizonunua baada ya kushuka katika daladala, niliamua
kununua matunda, matunda nk.
"Hapa naingia
ndani, haraka haraka na kutupa macho kitangani, ili tu nitimize azima yangu ya
kumziirishia mke wangu ukweli maana leo nikiondoka tena kama nilivyo fanya
mwanzo bado nitabaki kuumia mimi moyoni na kuzidi kukondeana na badae kufa na
kitu rohoni mwangu.
Lakini kwani ni nini
alichokikosa kutoka kwangu mpaka aamnue kubadilisha wanaume kama nguo.
Na kama aliamua hivi
si bora angeenda huko huko nyumbani kwa hawa wanaume au hata Guest kuliko
kufanya haya na kilia mtu anamuona tena bila hata aibu mchana usiku yeye ajali.
Mbaya hata mwanangu
snashuhudia uchafu huu kweli atakuwa na maadili gani katika maisha yake,
Leo na kesho anaanza
kuniletea wanaume ndani nitampiga au nitamuangalia tu.
Nimevumilia sana na
bado pesa namtumia za matumizi kumbe nampa nguvu ya kunisaliti na kumpunguzia
garama mwenye zamu siku hiyo.
Kweli mimi mjinga
najiona kabisa, lakini leo ndiyo mwisho wa ujinga wangu na ndiyo leo
nitaziirisha uanaume wangu nimdchokaaaaaaaa"
Nilijikuta nikiwaza
sana baada yakuwa nimekaa sebuleni kwangu huku nikifikiria jinsi ya kuingi kwa
fumanizi ambalo niliamini ni zairi liniumize sana moyo wangu kiasi kikubwa tu
kutokana na upendo niliokuwa nao kwa mke wangu kipenzi wa moyo wangu.
Niliamua kuinuka na
kuikagua nyumba yangu vizuri huku nikipitia mpaka chumba cha mwanangu
kumuangalia kama yupo lakini cha ajabu hakuwepo ndani hapo na ndipo nilipo
patwa na asira na kuamua kurudi haraka huku nikiwa na hasira mpaka nateteme
mwenyewe baada yakumuona mwanangu hayupo.
Nilichukua begi langu
na kuelekea ulipo mlango wa chumba changu na kuuchungulia kama utakuwa
umefungwa kwa ndani niliona hauja fungwa na ndipo niliamua kuufungua na kuingia
ndani bila hata kubisha hodi.
"Haaaaaaaaaaah
Mume wangu ni wewe!"
ITAENDELE.
..............