BORA NIENDE SEHEMU YA TISA
BORA NIENDE(9)
KING SOKA
PHONE:+255717758864
DAR ES SALAAM_TZ
PAGE
#STORY_ZA_KING_SOKA
Email address
jacksonsoka@gmail.com
ILIPO ISHIA→→→→→▼
Sikuweza kufahamu
nini kiliendelea pale.
Lakini baada ya
kuzinduka nilijikuta nikiwa nimechoka sana huku nikijishangaa ni wapi nilipo
kuwa.
Mpaka akili inakaa
sawa na kugundua nipo hosptali.
Nilistuka kutazama
saa na kuona ni saa tisa na dakika 34.
Mara bado sijakaa
vizuri simu ikaita ile napokea.
"Hallo"
Niliita mimi baada ya
kupokea simu.
"Upo wapi na
nakuitaji ufike ofsini haraka sana iwezekanavyo ukichelewa dakika kumi
tusionane wabaya"
Alimaliza kuongea mtu
alienipigia simu kutoka kazini.
ENDELEA nayo》》》》》▼
Niliamua kuondoka haraka wodini nilipokuwa
nimelala.
Nilichomoka kimya kimya bila hata kuaga na
kuvhukua ufunguo wa gari yangu ndogo,
Na kuiwasha huku nikitoka hosptalini pale kwa kasi
ya ajabu mpaka getini walishangaa kwa jinsi nilivyotoka na hakuna aliyejua kama
nini mimi ndiyo niliyetoka hosptalini katika wodi niliyokuwa nimelazwa mbaada
ya kuwa niechomwa sindano ya usingizi.
"Huyu boss naye anataka nini maana hizi
missed call alivyopiga kama ananidai banah au kisa sijatoa taarifa ya mimi kuto
kuuzuria leo.
Su kuna tatizo lililo jitokeza ofisini.
Nilijiuliza mwenyewe bila majibu huku nikiwa
nakimbiza gari kuwahi kama maagizo ya boss.
"Boss nimefika! Pia samahani kwa kukaa bila
taarifa hivyo naomba unisamehe kwanza kwa hilo"
Niliongea mimi baada ya kufika ofisini na kumkuta
boss akiwa ananisubiri huku uso akiwa ameukunja mpaka alionekana mzee kwa jinsi
slivyofura asira.
"Hapa hakuna cha samahani wala samabakuli.
Unajua hii kampuni sijafungua bila mahesababu au
usizani kuna siku mimi nakosa kujua mahesabu ya kampuni yangu hivyo siitaji
nini wala nini wala maeleze mengi siitaji hapa naitaji ni pesa zangu.
Ndipo mambo mengine yataendelea.
Yani siku mbili kukuachia majukumu umesha iba na
leo kujiona wewe ndiyo bosi mpaka kazini autaki kuja ili upate muda mzuri wa
kuficha pesa zangu.
Hivyo naomba haraka yani hapa una masaa kumi na
mbili nikute mahesabu yangu na pesa zangu mezani kinyume na hapo tutaonana
wabaya .
Mimi sifugi wezi mimi kama ni mshahara wako
nakulipa na bado uniibie"
Aliongea boss huku akinikaribisha na makofi mawili
yaliyoniuma sana mashavuni lakini sikuweza kurudisha sababu ndiyo boss tena
nikirudisha kazi sina , ilinibidi nivumilie tu.
"Boss mbona kama sikuelewi unamaanisha nini
labda!
Maana mimi toka lini nikahusika na masuala ya
hesabu na pesa mpaka leo pesa zipotee nihusike mimi.
Au kuna mchezo mnanichezea ili mimi kunifukuza
kazi kijanja, ni bora mniambie niondoke lakini siyo kunibambikia deni la
mamilioni wakati hata mimi hizo pesa sijawahi kuzishika leo itakuwaje niibibe
na wahusuka wa vitengo hivyo wapo wametulia tu wanasikilizia mimi sihusiki na
hata pesa zenyewe sina hata ukinipa mwaka "
Niliongea huku machozi yakinitoka maana sikuelewa
kinacho endelea kwa kile alicho kiongea boss.
Kwakuwa niliona mambo yamesha kuwa magumu.
Niliamua kurudi hospital ya Temeke na kumkuta
nessy aliyekuwa akimuudumia mgonjwa wangu ambaye akujulikana ni wakati gani
ataweza kuruhusiwa na kurejea nyumbani kwao.
"Samahani kwa usumbufu Dada yangu kwa hichi
ninachokuambia.
Hapa nilipo naweza nikasafiri kesho au hata leo
usiku.
Hivyo naomba nikuachie hizi pesa endapo sinta
safiri nitakuja lakini kama nikisafiri naomba umkabizi mwanamke huyu.
Na wewe uchukue laki tano.
Pia namba yangu ya simu hii hapa utaimpa pia.
Maana hapo alipo ana hata simu tena vyote tuliacha
katika eneo la ajali.
Niliongea huku nikiwa naimani kabisa uwenda sinta
rudi hospitalini pale tena labda baada ya muda.
Hatimaye niliondoka kuelekea nyumbani kwangu
ninapo ishi mimi na paka wangu.
Na baazi ya mifugo Kuku na Kanga.
Sikusmini baada ya kufungua geti tu, ile naingia
ndani hata mguu wa pili aujaingia ndani ya geti nilishangaa nikiwekwa chini ya
ulizi na askari waliokuwa wameongozana na boss wangu na baazi ya wafanyakazi
wenzangu.
"Unajua Jackson nilikuambia nakupa masaa kumi
na mbili ukawa jeuri huku ukinijibu kwa jinsi uwezavyo sasa nikaona dawa ya
kiburi ni jeuri.
Hivyo hapa kukuacha kwako ni wewe kurudisha pesa
zangu na siyo mambo mengine.
Kuna wenzako wana miaka saba mpaka kumi hawajawahi
kuiba lakini wewe ni miezi miwili unaanza kuiba"
Aliongea boss wangu
"Jamani mbona mnanione kiasi hiki nini
nilicho kukosea boss mpaka umeamua kunifanyia ukatili huu.
Mimi kweli naweza kuwa ni muizi wa ml75.
Boss embu fikiria vizuri tena ni vipi mimi naweza
kuusika na upotevu huo wapeza hizo jamani"
Niliongea mimi
Lakini hakuna aliye nisikiliza na kunifanya
nishindwa hata kuendelea kuongea na kuniamuru nifungue nyuba yangu waweze kuikagua.
Baada ya muda kila mmoja alitoka ndani akiwa
mikono mitupu .
Kwa kuashiria hakuna alicho kiona lakini boss
akutaka kuelewa zaidi alizamiria kunifikisha police.
"Afande kamata huyo peleka kwenye gari na
nyumba tunaifunga mpaka itakapo julikana tamati yake na funguo yake ndiyo
atakapo rudishiwa"
Aliongea askari aliyekuwa ndiye mku wa kikosi
kilichokuja nyumbani kwangu.
"Mimi siendi sehemu mbona napewa kesi nisiyo
ijua milioni sabini na tano ningechukua mimi kazini bingefuata nini kama siyo
ni uonevu huu.
Boss unanione mimi chinguza kwanza"
Niongea uku nikiburuzwa kuelekea kuelekea ilipo
gari ta police.
ITAENDELEA→→→→→