BORA NIENDE SEHEMU YA NANE
BORA NIENDE(8)
KING SOKA
PHONE:+255717758864
DAR ES SALAAM_TZ
PAGE
#STORY_ZA_KING_SOKA
Email address
jacksonsoka@gmail.com
TUJIKUMBUSHE→→→→↓
"Sawa nessy mimi
nitafanya kama inavyotakiwa.
Kwahiyo nifike hapa
saa ngapi.
Maana nakaa mbali
kweli nisije nikschelewa nikakuta mambo mengine tena.
Maana ya mungu mengi
dada angu"
Niliongea mimi
"Wewe cha
kufanya ni kuwahi asubuhi sana hapa.
Pia zingatia maagizo
kwa faida yako!"
SONGA NAYO▶▶▶▶▶▶↓
Aliongea nesy huku
akiniaga siku niliyo mpeleke mgonjwa hosptal ya temeke nikiwa hata simfahamu
lakini hospitalini walitambua kama mimi ni ndugu yake na mgonjwa.
"Sawa
nimekuelewa nitajitahidi nikutakie kazi njema.
Niliongea huku
nikigeulia mlango na kuondoka.
Hapo ndipo ilikuwa
siku ya kwanza kukutana na mke wangu mwanamke niliyetokea kumpenda kwa moyo
wangu na kujitolea mpaka maisha yangu ili apate kuishi.
Sikujali wali
sikuwaza nini kitakacho nitokea mbeleni zaidi ya kujali maisha yake kwanza.
Na wala sikufahamu
kama unge kuwa ni mke wa leo.
Hasubuhi na mapema
siku iliyofuata niliamka na kuchukua usafiri wangu kama ilivyo kawaida yangu
kwa kila siku.
Lakini siku hile
niliwahi sana kuamka ili niwahi hospital kumtazama mgonjwa niliye mpeleka usiku
uku akiwa ajitambui.
Hatimaye nilifika
hospital pale na kunyoosha moja kwa moja mpaka mapokezi na kusubiri, baada ya
muda nilimuona Nessy aliyenipokea usiku wa jana akitoka huku akiwa anakabizi
zamu kwa mwenzake .
Ili yeye aelekee
nyumbani kupumzika kutokana na kuwa zamu ya usiku.
"Habari yako!
Hafazali umewahi maana yani nilikua ndiyo nakabizi zamu kwa mwenzangu, na mimi
noondoke kuelekea nymbani lakini madamu umekuja hebu njoo huku kwa doctor
kwanza tuongee maana hali ya mgonjwa siyo nzuri sana"
Aliongea nessy
aliyenipokea j
Usiku nilivyokuja na
mgonjwa hospital hapo niliyemkuta akikaribia kuondoka nyumbani.
"Karibu "
Alitukaribisha Doctor
baada ya kuingia officeni kwake.
"Asante Doctor.
Huyu ndiye yule mwenye mgonjwa wa ajali wa jana usiku."
Aiongea nessy huku
akivuta kiti na kukaa.
"Habari yako
kijana vizuri sana kwa kuwahi.
Vipi umekuja na mtu
wa kutoa damu maana hali ya mgonjwa siyo nzuri sana na inaitajika damu ya
haraka sana kusudi aweze kupona.
Hii ni kutokana na
damu tuliyo muongezea ndiyo iliyomfikisha mpaka leo hii bado anapumua lakini
vinginevyo angelisha tutoka tokea jana kwa nyingi iliyokuwa ikimvuja kutoka
Kichwani, Mdomoni nk.
Utakuwa umefanya la
muhimu sana kwa kumsaidi mke wako"
Aliongea Doctor huku
mwisho wa maongezi aluongea kitu kilicho nishangaza kuambiwa mke wangu wakati
hata simfamu ni nimemsaidia tu.
"Doctor mtu
wakutoa damu kiukweli nimeznguka sana lakini nimekosa.
Niliongea mimi.
Lakini baada ya kuona
wote wamenyamaza kimya niliamua kuondoa ukimya ule kwa kusema mimi ndiye nitakayetoa
damu.
Kitu kilicho
washangaza Doctor na Nessy mpaka wote wakageuka na kuniangalia mara mbili mbili
kama awaamini kama naweza kutoa damu kwa ajili ya kimuongezea mwanamke yule
ambaye bado hata nilikuwa sijapata kumuona kwa sura hata sijui ni mweupe au
mweusi kutokana na hali niliyo mkuta nayo usiku wakati akiwa ameterekezwa
makorongoni.
"Doctor! Mimi
nitatoa damu mpaka imtosheleze mdonjwa huyu.
Naomba tu mnipe
maelekezo maana naona hamna muda wa kupoteza asije akatutoka wakati ameshafika
sehemu ya huduma"
Niliongea mimi huku
nikiwa natetemeka, lakini ilinibidi nijikaze.
Hatima zoezi la kutoa
damu likakamika na kuchukuliwa vipimo kwanza kabla ya kuongezewa kwa mgonjwa.
Damu ilikuwa salama
hivyo ilifaa kumwekea mgonjwa na ndipo mambo mengine yaendelee.
"Inabidi
upumzike hapa kwa muda kwanza usije ukazurika ukiondoka hivi sasa.
Maana kutoa damu siyo
jambo la kawaida tena kwa mtu ambaye hata ujajiandaa.
Inabidi upumzike kwa
muda usiyo pungua masaa manne mpaka saba"
Aliongea nessy baada
ya kumaliza zoezi la utoaji wa damu.
"Hapana nawahi
kazini maana hata ruksa sijaomba, mimi naomba mumuangalie kwa makini jamani
asije akapatwa na tatizo lolote jamani maana itakuwa hakuna nilicho kifanya na
hata Mungu atoweza kunisamehe.
Kwa kumpoteza mtu
huyu maana hata bado sijam..."
Nilikatisha kuongea
baada ya kujikuta nakaribia kuropoka kuhusu mgonjwa yule hata simfahamu.
Niliomba sana
kuondoka lakini nilizuiwa na badala yake nilipigwa sindano ya usingizi.
Kwa zumuni la nipate
kusinzia na nisiwasumbue madoctor na manesy katika kazi yao ya kurudisha uhai
wa mgonjwa wangu.
"Achomwe sindano
ya usingizi atulie, tofauti na hilo bado atasumbua na badae kutoroka na kututia
katika kashifa za uzembe"
Aliongea doctor
ambaye ndiyo nilimuona kwa muda huo kabla ya hapo nilikuwa sijamuona.
"Kwa nini
mnanifanyia hivi jamani mnajua mimi nitakosa kazi kwa ajili ya vitu kama hivi.
Istoshe kazini
penyewe ndiyo kwanza namiezi miwili leo nisiende, na hata taarifa yangu hawana
amuoni mnanitia majaribuni jamani mimi naonba niondoke tu kwa amani mbona damu
nimetoa kwa moyo wangu mweupe iweje kuondoka iwe tatizo au kuna damu ya
kuongeza mnitoe ili mniache niende kazini.
Mnazani mimi nitamkomboa
vipi m g o njwaaaa w a nguuuu"
Niliongea uku
nikizidi kulegea na badae kushindwa kuunganisha maneno na kujikuta naanguka
kitandani na kulala .
Sikuweza kufahamu
nini kiliendelea pale.
Lakini baada ya
kuzinduka nilijikuta nikiwa nimechoka sana huku nikijishangaa ni wapi nilipo
kuwa.
Mpaka akili inakaa
sawa na kugundua nipo hosptali.
Nilistuka kutazama
saa na kuona ni saa tisa na dakika 34.
Mara bado sijakaa
vizuri simu ikaita ile napokea.
"Hallo"
Niliita mimi baada ya
kupokea simu.
"Upo wapi na
nakuitaji ufike ofsini haraka sana iwezekanavyo ukichelewa dakika kumi
tusionane wabaya"
Alimaliza kuongea mtu
alienipigia simu kutoka kazini.
ITAENDELEA