KINGSOKA

KINGSOKA

BORA NIENDE SEHEMU YA SABA



BORA NIENDE(7)

KING SOKA
PHONE:+255717758864
DAR ES SALAAM_TZ
PAGE
#STORY_ZA_KING_SOKA
Email address
jacksonsoka@gmail.com

TUJIKUMBESHE KIDOGO↓

"Niache mbona unanizuia nini nisiongee we niache nikukumbushe maana najua hujui mke wangu nilipo kutoa au ni wapi ulipotokea ungelikua unajua using fanya haya hivyo niache niongee.
Usitake kunikorofisha sawa"
Niliongea huku nikiwa na hasira sana kiasi nilikua nikitetemeka wakati namkumbusha mke wangu jinsi ilivyokuwa.

ENDELE NAYO》》》》》↓


"Sawa mume wangu mimi natoka maana najua sina cha kuongea mbele yako na wewe ukanielewa, lakini kabla sijatoka naomba uache kuendelea na mambo hayo mume wangu kipenzi nakupenda sana naomba usiendelee kukumbushia mambo yaliyopita napiga na goti hili kwa kukuomba usiendelee kuongea inanifanya nikumbuke mbali sana na ndiyo sababu mimi nimebaki nikiwa sina ndugu.
Nakuomba Nakuomba mume wangu , niahidi utokumbushia hayo mume wangu"
Akiongea mke wangu

"Sawa siongei tena ondoka basi mbona bado unaendelea kuniwekea kiwingu hapa.
Au unataka niondoke uniwekee sumu nife ili upate kutanua na mume wak mpya.
Uliyemuona ndiye kila kitu kwako mpaka kumpa taulo langu.
Yani kila kitu changu mpaka ndala.
Ondoka bana ujue unanipandisha asira wewe mwanamke usitake nipate mada kesi kwa kukuuwa hivyo nitokee hapa haraka nikigeuka nisikukute"
Niliongea kwa harisa iliyokuwa na ukali ndani yake, hiyo yote ni kutaka mke wangu atoke mbele ya uso wangu, maana kila nilipo mtazama nilipatwa na hasira mpaka nilijikuta nikilia mimi pekeyangu .

"Sikutegemea mimi kama mke wangu anaweza nifanyia hivi .
Bora nilivyokuwa nikiambiwa na watu tu bila hata kushuhudia maana naweza kufa kwa presha kwa mtindo huu.
Mwanamke huyu alitaka nini kwangu akakosa mpaka aamue kunitenda hivi tena ndani kwangu.
Na jamaa huyu alijiamini nini mpaka akaingia ndani kwangu na kula tunda langu bila hata uoga huku akipepewa na feni kabisa yani kama yupo kwake.
Anafanya yake akimaliza anaenda bafuni kwangu nilipo oga na mke wangu leo anaoga yeye na mke wangu yani karisi nafasi yangu kabisa dah kweli hii dinia ulimwengu shujaa.
Leo ndani kwangu analala mwamaume na mke wangu huku mwanangu akiwa hayupo!"
Niliwaza

DAADA YA MAASAA MAWILI

"Nimemaliza kazi hivyo karibu chai ndipo nitoe hukumu yangu"
Niliongea mimi baada ya kumaliza kuoga na kila kitu hivyo nilirudi sebleni na kuketi chini ili nianze kuongea na mke wangu.

"Asante mume wangu lakini nimeshiba maana hata kula sitamani maana najuta mume wangu kwa hiki nilicho kitenda"
Aliongea mke wangu uku akiwa anaangaika utazani kiti kina miba.

"Unajua mimi siyo mjinga mke wangu hivyo kujutia ni sawa na kazi bure.
Pia naomba mnisamehe kwa kuwaingilia katika mapenzi yenu mliokuwa mkila starehe zenu.
Unajua naumia sana moyoni mwangu. Pia niwaombe samahani kwa yote.
Bwana mkubwa najua ufahamu mimi na mke wangu ni wapi tulipo toka.
Lakini wewe bila hata uoga leo umeingia katika nyumba yangu na kulala na mke wangu, najua leo siyo siku ya kwanza wala haitakuwa ya mwisho hivyo mimi nsona nikuache uendeleee na starehe zenu"
Niliongea mimi huku nikikaa vizuri kwa kujiamini.

"Kwa nini unasema hivyo mume wangu.
Mbona unafika mbali kiasi hicho"
Aliongea mke wangu.

"Najua uwezi kunielewa lakini utaelewa tu.
Maana nimechoka kuwa na maisha ya kujililia kila siku.
Nakumbuka sana mahali nilipotoka na wewe na ndiyo maana nashindwa hata kukupiga wala kukuhukumu kwa aina yoyote.
Mapenzi yanaumiza sana mke wangu hivyo sipendi ujutie kama mimi ninavyojutia mimi sasa leo.
Nazani jikoni ulikataa nisikuambie lakini sasa inabidi nikuambie tu.
Maana siwezi kuondoka bila kukuambia.
Pia naomba mnisikilize kwa makini maana hii leo ndiyo nazani inaenda kuwa itimisho"
Niliongea mimi

"Kabla ya yote naomba kujua mwanangu yupo wapi? maana tokea jana sijamuona hata mpaka sasa sijamuona"
Niliongea mimi
"Hapana mume wangu yupo kwa mama Abdalah.
Pia akitoka shule atakuja na hii ndiyo mida yake ya kurudi"
Aliongea mke wangu.

"Naomba mnisikilize kwa makini haya nitakayo yaongea.
Mke wangu nasiktika sana kukuambia mimi na wewe basi tena.
Maana siitaji kurudia matatizo niliyoyapita kwa sababu yako.
Na leo hii ndiyo mwisho wa kuishi na wewe nimeamua kuondoka na kwenda kuishi mbali kudpusha shari.
Unakumbuka siku uliyopatwa na ajali.
Nilikusaidia bila hata kujali ni mazingira gani uliyokuwepo, nilijitolea maisha yangu kukutolea damu ili upate kuishi naududi tena duniani uweze kuwatafuta wabaya wako.

"Kaka mgonjwa wako ana hali mbaya sana kama nilivyokuambia inabidi ufanye uwezekano wa kesho asubuhi uwahi hosptalini hapa ukiwa na mtu anaeweza kumtolea damu ili tuweze kuendelea na matibabu lakini bila damu hatuwezi kufanya kitu chochote kutokana na mgonjwa kuitajika damu kwanza.
Hivyo tunakusii uzingatie muda na pia jitahidi uwezavyo maana akiba yetu ya damu ni ndogo sana hivyo haiwezi kumsaidia chochote na kurudisha uhai wake kwa jinsi alivyovuja damu"
Aliongea nessy uku mkononi akiwa ameshika kitabu na glopsi akiwa anaelekea chumba cha wagonjwa mauti uti.

"Sawa nessy mimi nitafanya kama inavyotakiwa.
Kwahiyo nifike hapa saa ngapi.
Maana nakaa mbali kweli nisije nikschelewa nikakuta mambo mengine tena.
Maana ya mungu mengi dada angu"
Niliongea mimi
"Wewe cha kufanya ni kuwahi asubuhi sana hapa.
Pia zingatia maagizo kwa faida yako!"


ITAENDELEA→→→→→