KINGSOKA

KINGSOKA

BORA NIENDE SEHEMU YA 12



 BORA NIENDE(12)

KING SOKA
PHONE:+255717758864
DAR ES SALAAM_TZ
PAGE
#STORY_ZA_KING_SOKA
Email address
jacksonsoka@gmail.com



Niliipokea kwa haraka sana moyoni niliani itakuwa ni msichana yule niliye msaidia.

"Hallo"
Niliitika mimi
"Habari yako kaka.
Samahani natumauni naongea na Jackson"
Aliongea mtu alie nipigia simu.
"Ndiyo ndiye mimi wala ujakosea"

Nilimjibu
"Sawa ni hivi nazani unanikumbuka mimi ndiye mtu niliye nunua hiyo nyumba unayoishi sasa.
Hivyo kesho nataka kuamia naomba ufanye ustarabu wa mazingira ili niikute nyumba katika hali ya usafi na usalama pia.
Ikiwezekana hata leo uniletee funguo zangu hapa airport Jumbo bar"
Alimaliza kuongea ikiwa hata sijamjibu alikata simu.
"Vipi kaka natumaini hapo naongea na dalali wa nyumba vyumba na viwanja"
Niliongea mimi baada ya kuambiwa baada ya kuambiwa naitajika kuama katika nyumba yangu na aliye inunua anakuja kuishi na familia yake.
"Ndiyo unaongea na Ramadhan dalali mkubwa mpaka serikali inanitambua kwa kazi yangu huwa sibaatishagi"
Aliongea dalali kwa kujigamba huku akijisifia sana.

Basi dalali alinipatia nyumba ya kupanga iliyokuwa na vyumba viwili na seble choo cha ndani master nk.
Nikakipa kodi na kutafuta usafiri wa haraka kuamisha vitu vyangu ili nimpishe mwenye nyumba.

Baada ya wiki tatu nilipokea simu ya mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Melisa.

"Hallo samahani mimi ni Melisa msichana uliyenisaidia siku niliyopatwa na ajali.
Na kunipeleka hosptal Temeke .
Baada ya kupona nilipewa number yako na ness lakini hukuwa ukipatikana.
Hivyo juzi nilienda tena hosptal na kuomba namba yako nikaambiwa ulienda pale hosptal kuniulizia.
Kwanza nashukuru sana kwa msaada wako Kaka yangu maana kama siyo wewe nilikua nakufa.
Naweza kuonana na wewe leo kama hauto jali"
Aliongea msichana huyo upande wa pili wa simu.
Nilibaki nikiwa kama siamini ninacho kisikia lakini ilinibidi nikubakiand nae hata kwenda kumuona.
Nilimuambia naumwa hivyo anaweza kuja nyumbani kama hato jali.
Alikubali na kuniahidi mda mfupi ujao.
Ukweli nilikuwa siumwi lakini niliamua kumdanganya tu ili aje nyumbani na Ndiyo itakuwa sehemu sahihi ya kukaa na kuzungumza kuliko kukutana katika kumbi za starehe.

Baada ya kumaliza maongezi na msichana huyo simu yangu ilikuwa na ujumbe mfupi wa maandishi (sms)niliifungua na kuisoma nayo ilikua ni number mpya.
"Naona upo bize mda wote! Napiga unatumika tu hivyo ukimaliza nitafute sawa bwana mdogo"
Sms ilisoneka hivyo.
Kitu kilicho nifanya nibaki nikijiuliza itakuwa ni namba ya nani lakini nilikosa majibu na kusmua kuipotezea na kuendelea na usafi wa nyumba yangu hiyo niliyokuwa nimeamia mda siyo mrefu, nikiwa bado napanga vitu simu iliita tena.
Kunifanya niache nilichokuwa
nikikifanya na kuifuata simu.

"Hallo.
Niliongea baada ya kupoa simu.
"Mimi Melisa nilikua nikikuambia nishukie njia panda au kipawa maana nimesha panda daladala la gongo la mboto"
Aliongea Melisa baada ya kuwa amesha panda gari na kuwa anakuja ntumbani ninapo ishi mimi.
Nilimuelekeza ashukie njia panda na hapo atapanda tax zakuja karakara.
Lakini kwa wenyeji huwa tunatembea tu.

Baada ya muda mfupi akishawasili na kushuka katika daladala na kunipigia simu nilimuelrkeza na kuchukua tex mpaka nilipo kuwa nikimsubiri njiani maana kwa kumuelekeza ilikua ni ngumu mtu kufika mgeni.

Hatmaye alifika na sikuamini kama ni yeye kutokana na siku niliyomsaidia jisi alivyokuwa na sasa akivyo kuwa mzuri.
Mpaka walio kuwa wakipita njiani wakibaki kugeuka nyuma kwa jinsi.
Melisa akivyo jazia na alivyo kuwa na umbo zuri lililo mchanganya mpata dereva tax na kutaka kusahau nauli.

Baada ya kumuona tu nilijiapiza moyoni kuwa lazima awe mke wangu kwa jinsi nilivyo muona tu.
Nilitokea kumpenda kutoka moyoni.

"Karibu hapa ndipo nyumbani kwangu naishi peke yangu na mimi ndiyo baba wa nyumba na mama pia.
Hivyo jisikie upo huru ondoa shaka"
Niliongea baada yakuwa tumesha fika nyumbani.

"Inamaana haujaowa au unanitania jamani nikutwe humu ndani niaribiwe uso wangu"
Aliuliza Melisa.
"Ndiyo sijaowa kwani uamini kama sijaowa.
Na kwa nini nikudanganye sasa yani mimi naishi peke yangu na mgeni kama wewe basi ndiyo furaha yangu"
Nilimjibu huku nikiwa namuandalia juis ili tuongee vizuri uku akilainisha koo.

"Vipi za siku nyingi maana yakaribia mwaka sasa tokea siku niliyokuacha hospital.
Nilipata matatizo ndiyo maana siyo kama nilikuterekeza.
Na vipi ness alikupa mzigo wako nilimuachia ili ukipona uweze kukusaidia kwa muda ambao utakuwa bado ujaanza kazi"
Nilimongea mimi.
"Ndiyo alinigaiya.
Asante sana kwa msaada wako maana bila wewe leo mimi ningekuwa marehemu hivyo wewe ndiyo msaada wangu hapa duniani bila wewe sijui ningekuwa nini mimi"
Aliongea Melisa
Huku akiwa anafuta machozi kwa uchungu.
"Samahani kwa kukukumbusha machungu uliyokuwa umeyasahau nisamehe sana Melisa"
Niliongea mimi.
"Hapana Jack.
Unajua mimi hapa nilipo sijui hata ni mgeni wa nani na wewe naweza kukuambia maana wewe ndiyo msaada wangu hivyo inabidi tu nikuambie ukweli.
Mimi ni yatima na wazazi wangu wameuwawa ile siku uliyoniokota ndiyo siku pia wazazi wangu waliuwawa na kutupwa pia korongoni hivyo hata makaburi ya wazazi wangu sifahamu yalipo"
Aliongea Melisa.
"Nyamaza usilie basi jamani"
Nilimbembeleza baada ya kuona anazi kulia kwa uchungu.


ITAENDELEA.................

Maisha ni safari ndefu sana hivyo usikose kufahamu ni kwa nini Jack alishindwa kufanya chochote baada ya kumfumania mke wake.
Nyumba zina siri sana lakini leo Jack kaamua kuweka azarani ili mjifunze kitu