BORA NIENDE SEHEMU YA 15
BORA NIENDE(15)
KING SOKA
PHONE:+255717758864
DAR ES SALAAM_TZ
PAGE
#STORY_ZA_KING_SOKA
Email address
jacksonsoka@gmail.com
Sehemu ya kumi na nne
iliishia pale Jack na Melisa walipokuwa wakiongea na Jack akiwa na kitu anataka
kumuambia Melisa ambaye moyoni mwake alikua akimpenda lakini Melissa aliamini
Jack ni kaka yake.
"Leo naomba
uende nyumbani kwako ukaangalie chumba chako maana muda sasa ujaenda na kule
vibaka wengi wanaweza wakagundua haupo na wakapitia dirishani.
Niliongea mimi huku
nikia na lengo langu binasfi moyoni.
"Kweli lakini
mbona haraka hivyo.
Unamaanisha niende
alafu nirudi au niende nibaki huko huko"
Aliniuliza Melisa.
Tulikubalia na
hatimaye alikubali na safari ya kwenda kwake ilianza huku nyuma na ilielekea
kunua vocha kusudi usiku ukifika niwasiliane nae na kumuambia shida yangu inayo
nisumbua muda mrefu.
"Melisa vipi
mbona kimya sana au ukufika salama"
Nilimuuliza kwa
kutumia text.
Lakini sikuyaona
majibu kutoka kwa Melisa niliendelea kusubiri na baada ya muda iliingia text
katika simu yangu.
"Ooooooh! Kaka
nilikua kuoga ndiyi maana nimechelewa kukujibu text yako.
Samahani kaka"
Alinijibu Melisa text
huku akitumia neno kaka kitu ambacho kilikuwa kikinipa wakati mgumu jinsi ya
kumuanza kumueleza ukweli wangu wa jinsi ninavyo mpenda.
"Sawa ila kuna
kitu nataka kukuambia hivyo ni uamuzi wako tu kukubali au kuto kubali na pia
unaweza kuomba muda wa kufikiria"
Nilimtumia text
"Sawa kaka
niambie hicho kitu maana tokea asubuhi mpaka sasa bado ujaniambia lakini nahisi
huu ndiyo muda muwafaka wa kuniambia kitu ulichotaka kuniambia mdogo wako"
Alinijibu Melisa
wakati tukiwa tunachati
Nilimuuliza upo
tatari kuole kama yupo mtu akajitokeza.
Alikataa na kuniambia
mpaka mimi nitakapo mruhusu hivyo kwakuwa siku hiyo nilizamiria kumuambia
ukweli wa kila kitu ilinibidi nitimize azma yangu ili atakapo rudi apate
kunielewa nini kusudio langu na atambue kama nampenda na nipo tayari kuushi naye
kama mume na mke.
"Melisa nisamehe
sana kwa hili lakini ni bora nikuambie ukweli uliokuwa moyoni mwangu.
Melisa najua wewe
sasa unanichukulia mimi kama kaka yako na jana ulitoka kuniuliza ni kwa nini
sijawahi kukuita Dada.
Hivyo naomba utambue
ukweli wa moyo wangu.
Melisa mimi nimekaa
siku nyingi na wewe na pia nimekujua kitambia na kila kitu ujawahi kunificha
ukweli wako asilimia kubwa naujua.
Hivyo ni vyema
utambue hisia zangu mimi nakupenda sana Melisa na ndiyo sababu ya kushindwa
hata kukuita Dada.
Nipo tayari kukuowa
na kuishi na wewe ili tu, tusije kutenga na kifo ndiyo kitutenganishe.
Sina maana unijibu
leo au lazima ukubali hapana ni iyari yako na nitakusikiluza maamuzi yako"
Nilimtumia text ndefu
kiasi kwamba hata mimi baada ya kurudia kuisoma palikua na shuhuli kidogo kwa
jinsi ilivyokuwa ndefu.
"Mmmmh!
Sikutegemea kaka kama ipo siku utakuja kuniambia vitu kama hivi nitaanzaje mimi
jamani kwa jinsi navyo kueshimu jamani mbona matatizo hayaishi upande wangu.
Nilitegemea wewe
ndiye pumziko langu lakini leo unanitaka kimapenzi.
Kweli mimi sinta weza
ni bora nibaki huku huku nikiteseka lakini siyo kuolewa na wewe mtu
niliyekuchukulia kama ndugu yangu tena kaka"
Alinijibu text yangu
huku akionekana ajapendezwa na kitendo kile cha mimi kumtaka kimapenzi huku
yeye skinichukulia kama kaka yake .
Baada ya kuona text
yake akiwa ameijibu vile, niliamua kumpigia ili nimbembeleze maana nilikua
nikimfahamu ni jinsi gani alivyokuwa mrahisi wa kutokwa na machozi.
Nilipiga simu zaidi
ya mara saba ikiita mpaka inakata nila kupokelewa.
Ikiwa wiki moja
imekatika tokea siku niliyomuambia Melisa ukweli wangu kitu ambacho
hakufurahishwa nacho na kumfanya anichukie siku zote.
Mpaka wiki insisha
bila hata kubip wala kutuma mesegi.
Kipindi hicho kwa
uwezo wa Mungu nilifungua duka la chakula na mahitaji mengine muhimu kama vocha
soda nk.
Hatimaya siku nazo
zilizudi kusongambele bila kuwasiliana na Melisa.
"Hello Melisa!
Inamaana ndiyo undugu umevunjika au kuna kitu kingine.
Maana sasa ni wiki ya
pili na siku hata upokei simu yangu wala ujibu mesegi zangu.
Nisamehe kama
nimekuuz na kukukosea kwa maneno yangu.
Hivyo bakia na amani
tu na mimi nitatafuta mke wa kuowa japo wewe ndiye ulikua chaguo la moyo wangu
japo tuliweka undugu.
Najua ujui ni kwa
nini nilikuchagua wewe Melisa"
Niliongea mimi baada
ya kupiga simu na Melisa kuipokea kwa mara ya kwanza tokea siku aliyo ondoka
kwangu.
Na usiki nilipo chati
naye na kumueleza kama nampenda.
"Hapana kaka!
Hapana kaka! Huko ni kunionea na kunifanya niishi kinyonge na nibaki na majonzi
niliyokuwa nimeyasahau kwa muda sasa.
Unajua kitu ulicho
niambia kiukweli nimeshindwa kuwa na maamuzi mpaka sasa na ndiyo maana
nashindwa hata kuongea na wewe nabaki na kukuonea aibu tu"
Aliongea Melisa baada
ya kuwa nimempigia simu.
"Haina haja
Melisa mimi nitabaki kama ndugu yako na wewe .
Hivyo jisikie amani
tu.
Usinifikirie sana na
ndiyo maana nilikupa muda wa kufikiria.
Sasa iweje uniogope
na ndiyo sababu umeshindwa kuchat wala kunijulia hali kama kweli mimi kaka
yako"
Niliongea mimi.
"Hapana kaka
siyo hivyo"
Alijibu na kabla
ajamaliza maongezi simu ilikatika.
Baada ya simu
kukatika nilizani labda ni yeye amekata Lakin kumbe salio ndiyo lilikua
limekata.
Niliondoka nyumbani
kwangu majira ya saa kumi na mbili jioni kuelekea njia Panda airpot lilipo duka
langu.
Nikiwa ndiyo nimefika
tu dukani kwani hata kukaa sijakaa simu iliita.
Nukaitoa mfukoni ili
kuangalia ni nani anaepiga na ndipo niipokee.
Niliona ni namba mpya
na hata apo awali bado sikuwahi kuiona.
"Hallo"
Niliongea baada ya
kuipokea simu ile.
"Habari yako
kijana"
Sauti ya mwanaume
niliisikia baada ya kusiki hivyo moja kwa moja nilihisi ni Melisa labda ameamua
kumpa mpenzi wake namba yangu.
"Salama nani?
Maana hii namba ni
mpya kwangu"
Niliongea mimi
"Mimi ni bosi
wako unanikumbuka"
Aliongea mwanaume
yule aliye nipigia simu.
"Bosi
wangu?"
Niliuliza
ITAENDELEA..........
Unakosaje kufafamu ni
boss gani
Na anashida gani
Ungana na mimi mwanzo
mwisho