BORA NIENDE SEHEMU YA 14
BORA NIENDE(14)
KING SOKA
PHONE:+255717758864
DAR ES SALAAM_TZ
PAGE
#STORY_ZA_KING_SOKA
Email address
jacksonsoka@gmail.com
Sehemu ya13 iliishia
pale simu inaita naitaza ni namba mpya ambayo aikuwa na jina katika screen ya
simu yangu.
Haikujulikana
niliipokea au ni nani aliyekuwa akipiga lakini niliishia kuitazama tu.
ENDELEA
SASA...........
"Hallo"
Nilipokea simu na
kuitika.
"Hallo! Kaka
mbona unanifanyia hivyo jamani hata kujibu mesegi zangu ukaona tabu na simu
ukazima.
Umenifanya sijala
usiku kucha nikikuwaza wewe mpaka nilitamani nije huko usiku sema niliogopa,
kwanini lakini kaka umeamua kunifanyia hivyo ujue wewe ndiye ndugu yangu na
simuamini mtu yeyote zaidi yako"
Aliongea bila hata
kunipa nafasi ya kuongea mpaka alipo maliza kuongea alikua ni Melisa
"Hapana sikuwa
na salio na ndiyo maana nilishindwa kukujibu.
Usinifikirie vibaya
jamani .
Usilie utanifanya na
mimi nilie pia maana nafahamu ni jinsi gani ulivyo umia.
Nilimbembeleza na
hatimaye alinielewa na mambo mengine yaliendelea.
Siku zilizidi kusinga
huku Kaka na dada pia tukizidi kuwa ndugu kweli yani kama ndugu kweli lakini
kwa kila aliyepita na kutuona alijua ni mtu na mke wake maana mara nyingi
Melisa alipendelea kuja kulala kwangu huku kwake akuwa anaenda mara moja moja.
Lakini yote kwa yote
bado nilishindwa kuweka hisia zangu hazarani na kumtamkia Melisa ukweli kama
nampenda na namuitaki awe mama wa wanangu kwa jinsi nilivyokuwa nikimpenda na
kumueshimu.
"Melisa
nikuambie kitu maana.
Nimefikiria sana
lakini nimeona bora nikuulize ili nipate kufahamu masna isije siku likatokea
lakutokea, maana mimi ni ndugu yako hivyo napaswa kujua kila kitu kinacho
kuhusu wewe na wewe ujue kuhusu mimi.
Au nimekosea
Melisa"
Niliongea mimi huku
nikiwa namuonea aibu sana Melisa hata kumtazama machoni.
"Hapana kaka.
Pia kabla ya yote
naomba nikuulize kitu kwanza ili nijue tu.
Unajua mimi huwa
najiuliza sana hivi ni kwamba najipendekeza kukuita Kaka au maana hata siku
moja sijawi kukusikia ukiniita Dada kila siku upendelea kuniita jina langu tu
kwa nini?"
Aliongea Melisa huku
akinitazama sana machoni kwa macho makavu tasiyokuwa na hata chembe ya
kuweweseka.
"Hapana usiseme
hivyo unajua ipo siku nitakuita na pia ni history ndefu na siku nikikuambia
sababu sijui utajisikiaje au utanichikuliaje maana ungekuta nimesha kuambia
siku nyingi lakini nashindwa jinsi ya kukuambia"
Nilimjibu Melisa.
'Sawa bana
nitasubiri"
Aliongea Melisa.
"Melisa wewe na
mimi ni familia moja, hivyo naaomba kufahamu kama yupo mtu unampenda au
mnapendana na mnamalengo yakuishi wote mjenge familia nk.
Pia uweze
kunitambulisha ili nimjue siyo inatokea leo unaniongopea upo kwako kumbe upo
kwa mwanaume kweli sinta jisikia vizuri"
Nilimuuliza huku
nikiwa namtazama usoni Melisa
"Hapana Kaka
sina na siku nikimpata nitakuambia.
Lakini kwa sasa
siitaji mwanaume wa aina yoyote maana Kaka nitakapo jiingiza katika mapenzi kwa
sasa nitashindwa kuwa na malengo yangu, maana mama alikua akiniambia nikitaka
kutimiza malengo hivyo yangu niwaweke wanaume mbali na nililizingatia hilo
mpaka sasa sijawahi kuwa na mwanaume na simjui mwanaume wa aina yoyote katika
maisha mpaka sasa namiaka ishirini sijawahi kukutana na mwanaume"
Aliongea Melissa huku
akiwa abanitazama usoni bila hata aibu.
Kitu kilicho nifanya
niamini ni kweli maana hata nilipo muuliza alijibu bila hata kujiuma uma na
kupundisha maneno.
"Hakika Melissa
ndiye anayefaa kuwa mke wangu na kwa kuwa nampenda kweli lazima nimuambie
ukweli wa maisha yangu na hatimaye pia niweze kumwambia ukweli kama nampenda
ili nipate nafasi ya kuishi naye kwa amani.
Kama mtu ajawaho
kufanya mapenzi alafu nikimuacha sinta kaa nipate mke kama huyu kwa dunia hii
iliyojaa kila aina ya uchafu mpaka mtoto wa miaka tisa mimba anatoa"
Niliwaza nikimfikiria
sana Melisa ni vipi nitaanza kumwambia anielewe.
"Kaka unawaza
nini muda wote huo mpaka unanitusha.
Au unahisi
nimekudanganya, kama uniamini twende hospital tukapime ili uniamini siwezi
kukudanganya mimi na siku nikikudanganya au nikikukosea kosa kubwa naimani
kitakuwa ndiyo kifo changu kimewadia hata kama huto niazibu nitajiazibu
mwenyewe.
Nakupenda sana kaka
na wewe ndiye mkombozi wangu katika dunia na kila kitu nitafanya kama
unavyotaka, nikikukosea niazibu kama mdogo wako usiangalie umri na umbo"
Aliongea Melisa kitu
kilicho nifanya niamini kweli Melisa hajawahi kukutana na mwanaume kimwili,
maana kwa msichana alitewafahamu tayari wanaume ni vigumu kukubali kuwa muwazi
kwa kila jambo linalo muhusu ususani katika mapenzi nk.
"Sawa
nimekuelewa na nashukuru kwa kuyakabuzi mausha yako mikononi mwangu na mimi
nitakulinda mpaka mwisho wa maisha yangu au yako nakushidi sinto kufanyia
chochote kibaya na endapo nikikufanyia na balaa linikute mimi na siyo wewe
tena"
Nilimuuliza na mimi
kula kiapo changu juu ya Melisa na hapo ndipo harakati za kumuingiza melisa
katika imaya yangu zilipo zilipo anzia ni baada ya kujua vitu vingi vinavyo
muhusu.
Hatimaye wiki
ilikatika huku tukiwa bado ni kama ndugu.
Moyoni nikiwa na
mengi ya kumwambia lakini naona kama nitamkosea sana.
"Melisa
nikuambie kitu kizuri sana ambacho ni"
Niliongea mimi
"Nambie
kaka".
Alijibu
"Usikasirike
lakini maana"
Niliongea
"Sikasiriki bana
Kaka wewe niambie"
ITAENDELEA............
hapo sasa mtu mzima
anataka kuongea ukweli je araweza na kama akiweza atakubakiwa.
Mimi na wewe hatujui
subiri
Epsod ya 15
Ina majibu