BORA NIENDE SEHEMU YA 13
BORA NIENDE(13)
KING SOKA
PHONE:+255717758864
DAR ES SALAAM_TZ
PAGE
#STORY_ZA_KING_SOKA
Email address
jacksonsoka@gmail.com
ILIPO
ISHIA...........↓
"Hapana Jack.
Unajua mimi hapa
nilipo sijui hata ni mgeni wa nani na wewe naweza kukuambia maana wewe ndiyo
msaada wangu hivyo inabidi tu nikuambie ukweli.
Mimi ni yatima na
wazazi wangu wameuwawa ile siku uliyoniokota ndiyo siku pia wazazi wangu
waliuwawa na kutupwa pia korongoni hivyo hata makaburi ya wazazi wangu sifahamu
yalipo"
Aliongea Melisa.
"Nyamaza usilie
basi jamani"
Nilimbembeleza baada
ya kuona anazidi kulia kwa uchungu.
SONGA
NAYO..............
"Hapana Jack!
Usinifikirie mimi sana kama kulia nimeaha lia sana lakini mpaka leo sijapata
wakuniambia pol.
Unazani bila wewe
kunisaidia ni nani angenisaidia usiku uke na maporini kule.
Hivyo wewe ni mtu wa
samani sana kwangu na wewe ndiye ndugu yangu kuanzia sasa.
Maana siwafahamu
ndugu zangu na hata kwetu mkoani sipafahamu bali nafahamu ni Morogoro lakini
sifahamu hata mtu mmoja"
Aliongea Melisa huku
akizidi kutokwa na machozi kitu kilichofanya hata mimi nijisikie uchungu na
kusahau matatizo yangu nakuanza kumbembeleza yeye.
"Nyamaza usilie!
Uwezi jua Mungu anakusudio gani katika maisha yako.
Maana ni moja ya
mapito mazito uliyo yapitia pengine Mungu kuna jambo alilo kuepusha nalo lakini
wewe unaona ni matatizo na mzigo katika maisha yako.
"Hapana Jack!
Naomb tu niahidi kitu kimoja kama utakuwa ni ndugu yangu.
Yani Haka na Dada.
Maana hapa nilipo
nimebaki peke yangu na sina msaada pahalipo popote zaidi yako.
Maana hata hememu
ninapo kaa ni kwa sababu ya msaada wako bila wewe nisinge kuwepo mimi, hata
sehemu ya kuishi pia nisingekuwa nayo.
Nikushukuru tena kwa
msaada wako"
Aliongea Melisa huku
akiendelea kulia
Na hatima baada ya
maongezi muda mrefu, Melisa aliniaga na kutaka kuondoka.
Kwakuwa alikua ni
mgeni wangu na jinsi alivyokua ameumbika niliona ni vyema kuongozana nae huku
nikijifanya namtembeza ili afahamu mitaa, ili hata siku atakapo kuja tena
asiangaike kunitafuta nije kumpokea na kazalika.
Tulitembea taratibu
mpaka tukawasili njia panda airpot na Melisa alipanda daladala na atimaye
kuondoka zake Buguruni yalipo kuwa makazi yake.
Moyoni nilishaanza
kumpenda japo nilikua bado siamini kama ndiye yeye kweli niliye msaidia au lah.
"Kaka vipi"
Naona umeamua umlete
shemeji kwa miguu mpaka hapa kituoni badala ungechukua namba nilivyo mleta ili
nije kumchukua tena"
Aliongea dereva tax
alie mleta Melisa mwanzo wakati Melisa alivyo kuwa anakuja kwangu.
"Hapana kaka
nimeona nimtembeze ili atajue mazingira ili siku nyingine akija asipate tabu
kama leo"
Nilimjibu
"Sawa kaka
lakini hongera bana kwa kuchagua mtoto siyo haba kajahaliwa huyo siyo
mchezo"
Aliongea dereva yule
na mimi sikutaka kupoteza muda kutokana na jinsi nilivyokuwa na mawazo yangu.
Kichwani nilifikiria
sana mara ya pili msichana yule naambiwa ni mke wangu.
Doctor na Derava
moyoni nilicheka tu na kupuuzia nikaondoka nyumbani .
Hata kabla ajafika
nyumbani alinitumia mesegi
"Kaka nakupenda
sana na nimefurahi kuwa na kaka kama wewe.
Inabidi
nijivunie"
Sikuielewa text yake
hivyo nilirudisha simu mfukoni na kuendele murudi nyumbani taratibu huku njiani
nikiwa nawaza sana kivipi mimi naweza kuwa kaka yake wakati moyoni nimeshaanza
kumpenda.
Nilipitia bar kama
kawaida yangu na kuchukua nzinga wa konyagi ili nipate kunywa nikitoka huko
nikifika nyumbani nilale bila hata kupoteza muda.
Lakini nilishangaa
kushindwa kabsa kunywa siku hiyo huku nikimuwazia msicha yule huku nikiwa kama
namuona machoni mwangu Melisa akiwa ananikataza nisitumie kilevi kile .
"Hapana kaka
usitumie hicho siyo kizuri na kama unamawazo haina haja ya wewe kufanya pombe
ndiyo kimbilio lako cha msingi ni kujipanga na kujua ni vipi utalikabili
tatizo, na siyo kunywa pombe please Kaka acha nakuomba.
Ni sauti ya Melisa
iliyonijia ubongoni na kunifanya niamke huku nikiwa na mzinga wangu wa konyagi
na kumpa jamaa akiyekuwa amekaa kiti cha pembeni yangu.
"Vipi ndugu hali
tete au nini mbona kama umechemka vile.
Hii kitu siyo
mchezo"
Aliongea mtu yule
niliomfuata na kumkabizi mzinga ule wa konyagi.
"Hapana hauja
nishinda na hata kuufungua sijaufungua, ila nataka kuacha kabisa hivi
vitu"
Nilimjibu tu na
hatimaye niliondoka taratibu na kuanza kurejea nyumbani huku nikimfikiria sana
Melisa kuliko kitu chochote.
"Kaka jamani
mbona ujibu mesegi yangu au kuna kitu nimekuudhi jamani niambie nijue nakupenda
Kaka yangu kipenzi.
Mmmmmwaaaaaaaaah"
Alituma mesegi
nyingine Melisa.
Niliitazama tu simu
huku roho ikianza kuniuma.
"Endapo nitampa
ruhusa ya kuniita dada sindiyo nitakosa kabisa jinsi ya kumwingiza katika imaya
yangy wakati nimesha mpenda kama mpenzi wangu yeye kama kaka nifanyaje
kuipoteza hii kaka na dada ili nikamilishe lengo langu"
Niliwaza baada ya
kuisoma text ile ya Melisa.
Niliamua kulala bila
kumjibu kitu chochote.
Pia niliamua kuizima
simu yangu ili nilale tu kwa amani maana maisha yalikua yakinichanganya sana
nikaona hili la Melisa linaweza likanifanya kama kichaa kwa muda mfupi, kitu
ambacho sikutaka kitokee katika maisha na nilikua nikiomba sana.
Asubuhi nakuupuka
kitandani nawasha simu ili niangalie saa ndipo zinaingia msururu wa mesegi.
Wakati hata
sijafungua simu inaita.
Naitazama kwa makini
ni namba mpya isiyo kuwa na jina.
ITAENDELEA...............
Usikose kujua
kilichojiri sehemu ya 13
Je simu ni ya nani
iliyoingia ?
Je inahusu nini?.
Unaanzaje kukosa
labda