KINGSOKA

KINGSOKA

BORA NIENDE SEHEMU YA 11



BORA NIENDE(11)

KING SOKA
PHONE:+255717758864
DAR ES SALAAM_TZ
PAGE
#STORY_ZA_KING_SOKA
Email address
jacksonsoka@gmail.com

ILIPO ISHIA.........


"Hivi wewe unazani pesa inaokotwa 30000|-
Siyo pesa ya kutania kama utaki lete pesa yangu utambae zako kwanza usizidi kunichanganya hapa.
Maana hata sikuelewi kwanza unaguna kiuwizi uwizi naomba uniache tu nifanye kazi yangu mbona pesa yako ulivyotaja nimekupa bila pingamizi"
Niliongea mimi
"Unasemaje wewe mseng..."


Akiongea mwanamke yule uku akitokwa na matusi kinywani mwake kiasi kwamba nilishindwa kuvumilia na kumwambia sondoke zake tu maana ningeweza kumpiga hata makofi kutokana na jinsi alivyokuwa akinitusi matusi ya nguoni mengine hata kuyasema ni vigumu.

Asubuh na mapema niliamua kuondoka na kuelekea hospital nilipo muachaga mgonjwa wangu kabla ya kuingia matatizoni na boss wangu na hatimaye kunikamata na kunifilisi nyumba tangu.
Na ikiwa ni muda wowote inapigwa mnada.

"Habari yako dada mzma wewe.
Za siku nyingi!
Sijui kama unanikumbuka kwa kweli"
Niliongea baada ya kufika hospitalini pale na kumkuta Ness niliyemuachis mgonjwa wangu.
"Hapana sikukumbuki lakini sura kana nilishawahi kuiona sehemu, labda unikumbushe kidogo maana siunajua tena hapa hospital mambo mengi"
Aliongea Ness

"Ok! Asante kwa kunipa nafasi hii ya kuongea.
Mimi ni yule niliye mletega mgonjwa sliyekuwa amepatwa na ajali.
Lakini pia nilimtolea damu.
Na pia nilipata safari ya gafla hivyo niliondoka ikiwa mgonjwa wangu ajapona.
Hivyo kama unakumbuka kuna pesa pia nilikuachia umpe kama akipona na pia wewe nazani nilikupa kiasi kidogo pia"
Niliongea mimi nikiwa namkumbusha ness .
"Nimekukumbuka sana jamani tatizo umekonda sana alafu unanukia pombe kiasi kwamba japo umejitambulisha lakini bado kama siamini amini vile.
Tuyaache hayo! Za siku nyingi"
Aliongea ness kauli iliyonifanya nianze kuisi machozi yakinitoka.

Tuliongea mengi na kumuliza juu ya mgonjwa yule.
Nakuniambia alipona na kumkabizi kiasi kile cha pesa.
Ambacho akikua kikubwa lakini kwa matumizi ya kawaida ni kikubwa.
Kilikua ni milioni moja na laki tano.

"Nashukuru kama alipona.
Na je unawasiliano naye ya aina yoyote anbayo unaweza nisaidi kutapata.
Dada yangu maana hapa nilipo nina matatizo mpaka nahisi kichwa kupasuka.
Mimi siyo Jack yule uliyenifahamu kipindi kile niliyekuwa na gari zuri ya kutembelea na pesa ya kutumia aikuwa tatizo kwangu.
Lakini kwa sasa ni zaidi ya mateso bila saka"
Niliongea huku nikifuta machozi kitu kilichomshangaza sana ness na kuhisi ksma namuigizia vile.

"Jamani sasa mbona unalia!
Kama ni matatizo kaka yangu usilie ndiyo unayazidisha maana unavyolia unakumbuka mpaka ya nyuma ambayo yatakufanya uzidi kulia tu na hatimaye kukupa mateso makubwa ndani ya moyo wako"
Aliongea ness huku akichukua kikaratasi kilichokuwa na namba ya simu ya mgonjwa niliyempelekaga hospitalini hapo.

Niliondoka taratibu huku nikishindwa hata kutembea kwa jinsi ya nilivyokuwa nimekunywa pombe kupita kiasi na hatimaye nilidondoka barabarani pembeni umbali kidogo na ilipo hospital.

Kuja kuzinduka nilijiku nikiwa sina hata viatu wala shati nililokuwa nimevaa.
Huku mfukoni nikiwa sina hata sent ya kupandia dakadala na kurudi nyumbani kwangu kipawa nilipo kuwa nikiishi.
Niliondoka kwa miguu taratibu maana sikuwa ni jinsi tena kama pesa wakisha nisachi na kuchikua kila kitu.
Nilitembea kwa miguu temeke mpaka vingunguti ndipo nilipata lifti ya pikipiki.

Baada ya kufika nyumbani nilitafuta simu yangu iliyokuwa nyumbani kama simu ya mezani niliyopend kuitumia nikiwa nyumbani.
Nilichukua kikaratasi chenye namba lakini azikupatikana.
Nilipiga zaidi hata ya mara Hamsini nikijua labda ni usumbufu wa mtandao kama nilivyo zoea lakini haikuwa hivyo.

"Kesho nyumba yangu inauzwa.
Nitakuwa mgeni wa nani mimi yani nafilisika hivi hivi bila hata huruma.
Kwani nimemkosea nini mimi boss wangu mpaka aamue kunitesa kiasi hiki au kuna kitu nilicho kifanya"
Niliwaza na ndipo wazo la kutafuta nyumba ya kupanga ikanijina ili kuepusha shari na serikali.

Hatimaye nyumba yangu imeuzwa na mimi nikiwa bado sijapata nyumba ya kuishi.
Nyumba iliuzwa milioni 87 hivyo milion 12 nilipewa mimi na kupewa siku saba niwe nimesha hama kaika nyumba hile maana haikuwa mali yangu tena.

Wiki ya tatu namba aliyoinipa ness bado aipatikani.
Na mbaya zaidi hata dada mwenyewe simfahamu hata kwa sura wala jina hata ningekutana naye bado nisinge weza kumfahamu kutokana na siku niliyo msaidia alikua amechafuka damu sana usoni na mwili mzima kwa ujumla.

Hivyo niliamua nilirudi tena hosptal hili kuweza kutambua kana kuna uwezekano wowote wa kumpata msicha yule.
Nilifika na kumkuta ness yule tena akiwa anatoka nje ya geti la hosptal akiwa anarudi nyumbani.

"Samahani Dada kwa usumbufu.
Najua sasa upo nje ya kazi lakini pia naomba unisaidie maana wewe ndiyo msaada wangu.
Sina pakukimbilia ten, maana hata number uliyonipa aipatikani mpaka leo"
Niliongea mimi huku nikiwa nahema sana kwa kutembea mchana na jua kali.
"Jamani pole sana yani kaka angu sijui hata nikuambie nini maana sijui niseme ni mkosi au baati, yani unavyo niona hivi ndiyo nilikua niliongea naye na amesema ataelekea airport maana yeye anaishi vingunguti kwa sasa pia nimempa namba yako hivyo usijali atakutafuta.

Griiiiii griiiiiiii grii griii
Nilio wa vibration iliyokuwa ikiilia katika simu yangu ya nokia ya six batani.
Kutazama ilikuwa ni namba mpya iliyokuwa ikipiga.

ITAENDELEA...............

Kazi kazi maisha ni safari ndefu sana