KINGSOKA

KINGSOKA

.CHOZI LANGU(3)




Story..........CHOZI LANGU(3)
True story
Mtunz.......KING SOKA
Phone. .....0717758864/0786604915

"Jack unanionea.
Ingekuwa ingekuwa ni wewe ndiyo nakufanyia hivi ungejisikiaje? Au kisa mimi mwanamke ndiyo sababu ya wewe kunitesa kiasi hiki?
Au niende nikajiue pengine itakuwa ndiyo furaha yako.
Nikupende vipi wewe mwanaume? Nikupende vipi Jack, mbona unanitesa hivyo.


Kama kuwakata mwasichana wengi, mbona hata mimi niliwakataa wavulana wengi?
Sawa mimi nashukuru kwa yote mimi mnyonge tu"
Zai alikua akiongea kwa uchungu utazani akichokiongea kilikua na ukweli ndani yake.
"Zai hiyo gia yako uwezi kupanda mlima, umekuja na gia kubwa sana.
Ulimkataa nani kwa mfano.
Mbele ya macho yangu mlinyonyana mate, nikishuhudia lakini nilivumia na kujifanya sijaona kitu .
Ujiulizi nilikua na moyo wa aina gani?
Zai wewe siyo Zai wangu.
Nikikuuliza pesa zangu zilizokuwa Bank zipo wapi utajibu nini?
Uliomba laki moja ukaamisha salio lote.
Nilikuamini sana zaidi na zaidi, kumbe nilikua nikijipalia makaa kichwani bila mimi kujua.
Niache nilie kwani wakunifuta machozi, najua yupo na siku siyo nyingi nitampata.
Ulikuwa ni kama alamu yangu asubuh, hata usiku sikulala bila kuona meseji yako.
Umenifanya nikumbuke mengine, niliyokuwa nimesha sahau hata katika memory ya kichwa chabgu.
Kwa nini lakini umeamua kuja kutonesha kidonda kinachoanza kupona , kwa kukimwagia pilipili iliyo changanyika na chumvi.
Sikuchukii nasinadesturi ya kumchukuia mwanamke, japo uliniacha."
Nilijikuta nikitamani hata kumpiga makofi Zai lakini hata nguvu sikuwa nzao.
Mapenzi yanauma , na yanatesa.
Nilikumbuka mpaka msemo wa kaka yangu pindi alipogombana na mpenzi wake.
"Ni bora kukosea kujenga nyumba, kuliko kukosea mke wa kuoa"
Nilijikuta nikizidi kukumbuka mbali.
Tena kumbukumbu ilizidi kurudi nyuma mpaka siku niliyokutana na Zai kwa mara ya kwanza.

Naama 2009
"Kaka mambo"
"Poa vipi?"
"Fresh"
"Karibu"
"Asante, mmh nimeagizwa na bi mkubwa soda mbili.
Pesa atakuletea"
"Bi mkubwa wako ni yupi mbona simfahamu"
"Hahahaha, acha utani bana mimi nakaa ndani humu ujawahi msikia Zai Zai akizungumziwa.
Basi kama umeshikia ndiyo mimi"
"Oook poa soda mbili"
Ilikua ndiyo mara ya kwanza mimi kumuona Zai japo nilikua nikisikia akiongelewa saba na marafiki zangu.
Mpaka wazazi wake pamoja na majirani waluokuwa wakimdahamu.
Aikichukua mda Zai alirudi tena njee, safari hii slukua ameshika noti ya shilingi elfu kumi.
Aliniomba chenchi, japo nilikua nina chenchi chache lakini nilijikuta nikiwa kama mkate ndani ya chai,

ITAENDELEA............
like share like share
Unajua nilifanyaje usikose

king soka

Kwa urahisi wa kusoma simulizi zangu, nakushauri ulike page kwa kutumia hii link.

( https://www.facebook.com/Story-Za-King-Soka-521558664665742/# )