KINGSOKA

KINGSOKA

CHOZI LANGU(4)

Story..........CHOZI LANGU(4)
True story
Mtunz.......KING SOKA
Phone. .....0717758864/0786604915


Niliongia katika droo uki nikiwa namtazana sana machoni Zai.
Niliokota chenchi zote na kumkabizi yeye, pasipo kuchukua hata pesa aliyokuja nayo, kwa jinsi nilovyokuwa nimezimika kwake gafla tu.


Baada ya kumpa chenchi aliondoka, na mimi kwa kuwa nilipenda kumuona haraka haraka niliingia ndani kusudi nimchungulie kwa dirishani.
Nilimtazama mpaka alipo ingia ndani, ndipo na mimi nilirejea dukani kuendekea na mambo mengine.
Huku nikiwa napiga mahesabu ya vitu vya kuongeza, ili niagize mzigo.

Baada ya muda kaka alikua amekuja, tayari kwa kwenda kuagiza bidhaa za dukani.
Ndipo katika mahesabu niligundua kama sikuchukia pesa kwa Zai baada ya kumpa chenchi.
Nilitamani niende kwao, lakini niliofia kaka kunihisi vibaya.
Hivyo nilichukua pesa yangu na kujazia pale, kisha nikampa kaka pesa ya kwenda kuagiza mzigo.

"Hivi ni kweli sikuchukua pesa kwa Zai, au kuna sehemu nimeiweka.
Dah! Hii imeshakuwa kazi sasa, yani mara ya kwanza napagawa hivi je siku zijazo sitijikuta ninemaliza duka lote kwa mambo haya.
Hapana! Hii ndoto siyo nzuri hata kidogo"
Nilibaki nikiwaza peke yangu huku nikiwa najiuliza maswali bila majibu.
Nilihisi kutingishwa mabegani , mtu akuwa nyuma yangu sikuweza kutambya kwa haraka.
Kugeuka nilimkuta ni Zai, msichana aluouteka ufahamu wangu kwa haraka kuliko kawaida.

"Mbona unaonekana unamawazo sana.
Tatizo nini ?"
Zai aliuliza kwa sauti ya taratibu huku akiwa amenishika begani.
"Hapana nipo sawa mbona, sema siunajua bindamu sisi kuangaika .
Hivyo lazima niwaze maisha yangu sasa, kutegemea ndugu napo siyo kuzuri"
Nilimjibu, japo jibu nililomjibu ni tofauti na ilivyotakiwa nimjibu.
"Sawa kama hakuna unacho waza, lakini mimi natambua umenificha kitu.
Ila ungeniambia ningeweza kukusaidi gata kimawazo nk."
Zai alitoa noti ya Elfu kumi na kunikabizi, ukuakinuambia nipunguze mawazo.
Asijue kama sikua na mawazo yoyote, ika yeye ndiyo chanzo cha yote.
"Unasema una mawazo, mbona ulinipa chenchi bila kuchukua pesa?
Haya mimi nimekurudishia wengine je?
Kuwa makini kijana"
Zai aliongea huku anaondok, kurudi ndani kwao.
"Zai"
Nilimuita lakini baada ya kugeuka nilikosa hata cha kumwambia, zaidi nilimwambia asante kisa aliondoka zake.
Kama kawaida yangu nilikimbilia tena ndani, ili nimtizame kwa dirishani.
Lakini kumbe na yeye alikua amesha ustukia mchezo wangu.
Nilipofungua pazia tu, macho kwa macho yaligongana.
Nilikosa hata cha kuongea huku nikiwa na aibu chungu nzina, ilinibidi kufunga pazia kisha kueudi dukani.
Narudi dukani nakurana nate tena, uku akiwa ananitazama sana machoni.
"Mungu wangu nimekwisha, ni nini kilichonituma kuchungulia dirishani?
Hapa kaka akitokea akinistaki kw Kaka , na kaka anavyopenda sifa leo nitapigwaje Mungu wangu.
Bora nimuombe samahani kabla hayajawa makubwa"
Niliamua kutoka ili nimuombe msamaa.
Lakini natoka tu na kaka naye alikua anesha wasili, kutoka duka la jumla kufungasha bidhaa.
"Mungu wangu"
Nilistuka mpaka kaka alitambua hilo.
"Unastuka nini"
Kaka aliniuliza.
Nilikua nikitetemeka sana

ITAENDELEA........