KINGSOKA

KINGSOKA

CHOZI LANGU(1)

Story..........CHOZI LANGU(1)
True story
Mtunz.......KING SOKA
Phone. .....0717758864

ANZA SASA

Ni siku ambayo sitaki kuilumbuka katika maisha yangu.
Kila ninapo karibu kusahau, najikuta nakumbuka na machozi unitoka.
Nashindwa kuamini kama ni wewe uliotamka kwa kinywa chako.
"Jack nakupenda"
Leo upo wapi ule upendo wako.
Umesahahau kama mimi nilifukuzwa nyumbani, nikalala makorongoni katika mifereji ya maji machafu.


Nilipigwa nusu kufa, nikitetea uhai wako.
Uliniahidi mimi na wewe mpaka kuzikwa.
Unakumbuka siku ile niliyomwagiwa mafuta ya moto na dada yako?
Akidai mimi nakufanya utulii nyumbani.
Nikifikiria nina siku nne sijaonana na wewe, nilikubali lawama zote.
Hata kaka yako alivyo nipiga na narafiki zake, mpaka nilishindwa kutembe .
Umenifabya nitamke adharani nayachukia mapenzi, mpaka sasa kila anaeniambia ananipenda naona kama ndiyo wale wale.
Zai kweli wewe ndiyo niliyeiba pesa za kaka yangu milioni nne kwa ajili yako!
Au siyo Zai wewe.
Umenifanya mpaka sasa marafiki zangu wananiuliza kwanini kinondono siendi tena.
Ikiwa ndiyo sehemu nilipo kuliia.
Naogopa kukuona ukiwa na Issa, nitajitonesha kidonda kibachoanza kupona taratibu.
Kweli penzi la fukara ni mateso lakini yangu yamenizidia mara dufu.
Penzi lako limekuwa ni chanzo kikubwa cha maisha yangu kunyumba.
Na kuonekana kama kituko mbele za watu.
Zai ni kweli ukunipenda au ulipenda kunichuna kisa nilikua dukani?

2009
"Jack nakupenda sana, amini nakiambia na sipo tayari kuona upendo wako unapotea"
Aliongea Zai siku ambayo nilikua nimekaa naye tukipiga story nyingi sana.
Lakini leo ndiyo hayupo na mimi.
Ameondoka na kuniachia pecha kama chanzo cha machozi kwangu.
"Zai natambua unanipenda na mimi nakupenda sana.
Na naima wewe ndiyo furaha yangu maishani.
Nakuomba usiwe chanzo cha machozi yangu."
Nikiongea mimi nikiwa nimemshika Zai mkono, tukiwa tunajiandaa kwenda kunumua chips.

ITAENDELEA. ............

Naam Usikose kufuatilia mtiririko huu wa matukio ya kweli katika safari nzima ya mapenzi.
Ya kijana alitokea kujitolea kila kitu kwa mchana Zai lakini sasa anaijutia nafsi yake.
Cha kufanya ni wewe kila siku asubuhi saa mbili itakuwa ikiruka.
Na usiki kama kawaida ni Najma mwanza mwisho.
Na pia itakuwa fupi hivi hivi.
Mpaka itakapo fika mwisho wake.
TRUE STORY 2016

Kwa urahisi wa kusoma simulizi zangu, nakushauri ulike page kwa kutumia hii link.