KINGSOKA

KINGSOKA

TUNAPENDANA


Story..........TUNAPENDANA(1)
Mtunz.......KING SOKAPhone. .....0717758864
Page..........
Hadithi Kali Za KingSoka

Sikuwahi kufikiria kama na mimi ipo siku, na mimi nitampenda msichana kama ninavyopenda sasa na kunifanya niyafuraiye maisha ya mapenzi.
Nilishalizwa sana mpaka nikatamka hazarani sintokuja kupenda tena, nilidiriki hata kula kiapo juu ya mapenzi na kuwa mstari wa kwanza kuyaponda mapenzi kwa aina yoyote niliyojua mimi.




Ilifikia kipindi mpaka marafiki zangu walinitenga, na kunihisi uwenda tayari nimeshaingia katika mchezo mbaya wa jinsia moja.
Nakumbuka niliishi kwa tabu sana huku manyanyaso matusi na kejeli zikiwa ndani ya maisha yangu.
Hata shule niliyokuwa nikisoma nayo niliiona chungu , na yote ni kutokana na marafiki zangu pamoja na bahadhi ya wanafunzi waliokuwa wakiniandama na maneno machafu na yasiyo stahili hata ndani ya jamii ,kuyatamka hazarani"Jack ! Toka hapa sisi atukai na mtu asiyekuwa na demu(mpenzi) Hata siku moja atusikii skendo zako.
Wenzako kila siku wazazi wetu wanakuja shule kusikiliza kesi zetu, wewe masaa yote upo pekeyako pekeyako .
Au wenzako wanakunani nini( ..)"
Iliniuma sana hiyo siku mmoja wa wanafunzi alivyo nitamkia maneno hayo hazarani tena mbele za wanafunzi wengi wakike na wakiume.
Nilijiona ni kama nimejinyea huku nikitamani hata aridhi ipasuke niingie nisionekane, kuliko kuendelea kuishi shuleni pale.
Ukizingatia ilikua ni shule ya boading.
Kweli mapenzi nilikua nikiyachulia sana tena zaidi ya sana.
Hata pia baada ya kutengwa na marafiki zangu lakini bado msimamo wangu ulikua pale pale.

"Jack nakupenda! "
Ni sauti ya msichana aliyekuwa mrembo mpaka wanafunzi wote wa kiume walikua wakimtolea macho kutokana na umbo lake, shepu na sehemu zake kuwa na hipsi akitembea lazima ugeuke nyuma.
Aliongea siku moja niliyokua nimekaa chini ya mti nikitafaka ni lini nitamaliza shule na kuondokana na manyanyaso ya shuleni hapo.
Hata alipo niambia ananipenda nilijikuta nikimtizama tu bila hata jibu kumpa, kwani nilihisi moja kwa moja atakuwa ametumwa na marafiki zake, na kama siyo marafiki zake niliamini yaweza kuwa ni wale marafiki zangu walionitenga wakihisi mimi siyo rijali( siyo mwanaume niliye kamilika).
Nilijikuta machozi yakinitoka, nikiamini msichana yule alikua akinipima imani au ni njia ya wao kujua kama mimi ni rijali au lah.
"Dah! Imefikia mpaka atua naanza kuchunguzwa, au hawa jamaa wanataka nini kutoka kwangu jamani.
Kwani mimi nimekuja hapa kufata wasichana au kutafuta masomo? Mbona nazalilika kiasi hiki mimi nifanye nini mimi kuinusuru heshima yangu"
Nilijikuta nikiongea pekeyangu, huku machozi yakinitoka, kitu ambacho kilinifanya nikumbuke mbali na niwaze mambo mengi kuhusu mapenzi.
Nilikumbuka hata usemi wa kaka yangu mara ya mwisho wakati nasafiri kuelekea shule.

"Mdogo wangu soma kwa bidii, sasa unaingia shule ya sekondari na siyo ya msingi wala ya awali.
Huko utakunata na kila aina ya vitu, kuna starehe , ubabe, wizi, matusi, na kila aina ya matendo mabaya, hiyo ni kutokana na kuwa na wanafunzi waliokuja shuleni pale kwa sababu ya mapenzi, huku wengine wakija shukeni pale kwa sababu ya kuwaibia wenzao waliokuja na vitu vya thamani.
Vile vile wewe sasa zingatia kilicho kupeleka shule , kama ni mapenzi sawa matokeo yake utayaona siku ya mtihani"
Aliongea kaka yangu Noeli . Kisha mimi nikapanda gari na safari ya kuelekea shule ilianza .

"Jack! Yani mimi kukuambia nakupenda ndiyo kumekufanya ulie na uongee maneno uliyokuwa ukiyaongea , au kuna sababu nyingine .
Kama ipo unaweza kuniambia ilinijue na mimi , uenda nikawa msaada kwako hata kama siyo wa pesa hata mawazo"
Nilibaki nikimtazama usoni nikikosa hata jibu ya kumpa , maana asilimia mia niliamini ametumwa kunichinguza.
Maana kwa jinsi alivyokuwa alafu aje anifuate mimi ilikua ni ngumu kuamini .
Nilibaki kumtazama tu nilikosa hata cha kuongea.
Nilibaki nimeinama chini nikifikiria nimtukane au niondoke mahali pale"

"Sawa nimekuelewa.
Naomba nipe mda nifikirie maana upendo siyo jambo la kukurupuka haraka naweza nikaja kujutia huko mbeleni"
Nilimjibu kisa nikainuka sehemu niliyokuwa nimekaa, na kuondoka mbali kabisa ili nikakae pekeyangu niweze kufikiria mambo yangu ya badae.

Nilimfikiria sana msichana yule bila kupata jibu sahihi.
Kama ni kweli ananipenda au ametumwa kunichinguza kama mawazo yangu yanavyo nituma.
Kumbe hata baada ya kuondoka shuleni pale na kwenda mbali na eneo la uwanja wa shule, bado kuna wanafunzi waliojigawanya katika makundi ,walikua wakinifuata nyuma nyuma.
Ili watambue ni wapi ninapo elekea, sikujali sana maana niliamini nirahisi kwa mimi kuwapoteza maana vichaka vingi nilikua nikivifahamu.
Niliendelea taratibu na kisha kuingia kwenye moja ya kicha , na kuanza kutembea nikitambaa kama mtoto anaeanza kutaka kutembea, mpaka nilipo amini nimewapoteza nilianza taratibu kurejea shule, maana tayari nilishaona kule porini siyo pazuri kwa mimi kuendelea kuwepo kule.

"Inamaana ametupotea kweli ! Mbona kama masihara yani kirahisi hivi mtu anstupotea au ni mchawi mwenzetu.
Tusije tukaanza kupotea mmoja mmoja huku porini , turudini shule tu."
Aliongea mmoja wa wanafunzi waliokuwa wakinitafuta porini nisijue hata walikua na shida gani na mimi.
"Anabaati sana yani leo tungemkuta huku sijui angetuambia maana naasira nae sana huyu jamaa"
Akiongea Fred mwanafunzi niliyekuwa na ugomvi naye tokea siku naingia shuleni alionyesha kunichukia.

Nilijificha kisha wakapita tena na mimi nikaendelea kukimbia ili niwahi kufika shule ili hata watakapo fika wanikute nimekaa.
Niliamini ni njia moja ya kuwatisha uwenda wataniogopa wakihisi mimi mchawi nk.

"Hivi kweli wewe unanipenda mimi? Au kuna kitu unataka kujua kutoka kwangu, kama unanipenda nitaamini vipi.
Na mbaya zaidi shuleni nimehusiwa kusoma na siyo mapenzi, naweza nikakupenda lakini ukaja ukautesa moyo wangu na kunifanya nibaki na majonzi, kila siku niwe nalia tu ndiyo maana siitaji mpenzi , nisamehe kama nitakuwa nimekuudhi.
Ila uwo ndiyo wangu msimamo samahani kwa hilo"

ITAENDELEA. ...........

KING SOKA KWA MARA NYINGINE TENA ANAKUJA NA KIGONGO KIPYA tunapenda.
Simulizi hii ya TUNAPENDANA mwisho itakuwa na maswali mengi kwa wewe mpenzi na mpenzi wako lengo ni kukuelimisha na kukufundisha usicho kijua.

Naama king soka