Mkurugenzi ampigisha deki Mwalimu Mwanza
Mkurugenzi Misungwi, Mwaiteleke adaiwa kumuamuru mwalimu kudeki darasa mbele ya wanafunzi baada ya kukuta madarasa ni machafu
Habari
kutoka gazeti la Tanzania Diami imedai kuwa jana October 20 2016
mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Eliud
Mwaiteleke ameingia kwenye kundi la wakurugenzi wanaowanyanyasa na
kudhalilisha watumishi wa chini baada ya kudaiwa kumuamuru mwalimu wa
shule ya sekondari ya Shilala, Hamis Sengo, kudeki darasa zima, mbele ya
wanafunzi wake.
Inaelezwa
kuwa mkurugenzi huyo alifika shuleni hapo akiwa na watendaji wengine wa
wilaya na kukuta madarasa yakiwa machafu, ndipo aliamuru mwalimu huyo
kudeki darasa zima mbele ya wanafunzi wake, jambo ambalo limepingwa
vikali na kulaaniwa na chama cha walimu ‘CWT’ wilayani humo.