Michezo Suarez kataja sababu ya kwa nini anasema hawezi kushinda Ballon d’Or daima
Jina la Luis Suarez wa FC Barcelona
limegonga headlines tena baada ya kuripotiwa na mtandao wa ESPN kuwa
Suarez anaamini hawezi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia maarufu
kama Ballon d’Or huku akitaja baadhi ya sababu zake.
Suarez amesema hayo baada ya kukabidhiwa
kiatu cha dhahabu na wengi wakihoji baada ya tuzo hiyo ya ufungaji bora
wa Laliga mwaka 2015/2016 vipi anaweza akapewa nafasi ya kuwania tuzo
ya mchezaji bora wa Ulaya?
“Ballon d’Or ipo kwa ajili ya
masuala ya biashara yaani mtu anayefanya vizuri zaidi sokoni kuliko
mafanikio ya uwanjani, nimeshinda tuzo zote ikiwemo ya ufungaji bora
hiyo huwa haina ubishi kwa sababu anapewa mtu aliyefunga magoli mengi
hivyo hiyo mtu hawezi kuninyima, Ballon d’Or inaagalia mtu anayeuza mimi
siuzi malengo yangu ni kushinda Champions League”