KINGSOKA

KINGSOKA

Kocha kaeleza sababu za Drogba kukataa kucheza mechi ya Jumapili








Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Ivory Coast ambaye amewahi kuichezea klabu ya Chelsea ya England kwa mafanikio Didier Drogba ameingia kwenye headlines baada ya kugoma kuichezea klabu yake ya Montreal Impact katika mchezo wa Jumapili.

Kocha Mauro Biello anayeifundisha Montreal amethibitisha staa huyo kutoridhia kucheza katika mchezo dhidi ya Toronto akitokea benchi “Nilizungumza nae Jumamosi lakini alionekana kutoridhia suala la kutokea benchi na kucheza kwa dakika 18 za mwisho, hivyo akaona bora hasicheze kabisa”



Drogba alitaka kuanzishiwa benchi kutokana na kurejea akitokea majeruhi hivyo kocha hakutaka aanze kikosi cha kwanza moja kwa moja, kitu ambacho hakikumpendeza Drogba, staa huyo alijiunga na Montreal 2015 akitokea Chelsea na amefanikiwa kuichezea mechi 35 na kufunga magoli 21.
Katika mechi nne za mwisho za Montreal Drogba ametolewa katika mechi mbili, klabu ya Montreal inayoshiriki Ligi Kuu Marekani Major League ililazimishwa sare ya goli 2-2 na Toronto. Drogba kwa sasa ana umri wa miaka 38 na yupo katika hatua za mwisho za kumalizia soka lake la ushindani.